Azam FC inaendelea na
maandalizi ya siku saba jijini Nairobi, kesho watacheza mchezo wake wa pili
dhidi ta SOFAPAKA ya Kenya kwenye Uwanja wa Nyayo.
Kocha mkuu wa Azam
FC, Stewart Hall amesema mechi itakuwa nzuri kwake kutokana timu hizo kucheza
mchezo wa aina inayofanana baada ya kuzifundisha timu hizo.
Stewart alisema mechi
hiyo muhimu kwake itakuwa na sura tofauti kwa kukutanisha wachezaji walipata
mafunzo kupitia kwake, hivyo mbinu na aina nyingine ya mchezo bado SOFAPAKA
wanaitumia.
"Nataraji kuona
wachezaji wangu wote wakifanya vizuri hasa wa Azam FC, kupambana na timu
uliyoifundisha kunakuwa na ugumu, wanaweza kucheza wakifanana kila sehemu hali
itakayopunguza idadi ya magoli kwa moja timu hizo” alisema Stewart.
Alisema wachezaji
wake wanaonekana kucheza vizuri kipindi hiki, wamezoea hali ya hewa Nairobi
hivyo mchezo na SOFAPAKA watakuwa na kila sababu ya kufanya vizuri.
Naye Kocha wa
SOFAPAKA David Ouma alisema kukutana na Azam FC katika mechi ya kirafiki
ilikuwa moja ya mipango yao, wanatajia kucheza mchezo wa ushindani zaidi na
kuwapa nafasi wachezaji wake wapya walisajiliwa hivi karibuni.
“Haya ni maandalizi
mazuri kwa timu yangu, tumeanza mazoezi wiki mbili zimepata, kupitia mechi hii
tutajua maendeleo ya timu, wachezaji hasa hawa tuliowasajili, pia tutazidi
kujenga urafiki mzuri na Azam FC” alisema kocha Ouma.
Azam FC baada ya
mchezo huo, siku ya Jumatatu itapumzika kwa kufanya mazoezi, na kumaliza mchezo
wake wa tatu siku ya Jumanne dhidi ya K.C.B utakaochezwa kwenye Uwanja wa City
uliopo jijini hapa.
Timu hiyo inatarajiwa
kurejea jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano ikiwa ni siku mbili kabla ya
kuanza kwa ligi kuu Tanzania mzunguko wa mwisho wa ligi utakaoanza Jan 26 mwaka
huu.
0 comments:
Post a Comment