
Mzunguko wa pili ya Ligi Kuu ya
Vodacom utaanza Januari 26 mwaka huu huku kukiwa na maombi ya televisheni ya
SuperSport kuonesha mechi za Super Week kama ilivyokuwa katika mzunguko wa
kwanza.
Raundi tano za awali katika
ratiba ya mzunguko wa pili zinabaki kama zilivyo wakati nyingine zilizobaki
zitatolewa baada ya kuingiza mechi za Super Week.
Wakati huo huo, mzunguko wa pili
wa Ligi Daraja la Kwanza unatarajia kuanza Januari 26 mwaka huu. Ratiba ya ligi
hiyo na tarehe rasmi ya kuanza itatangazwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Ligi
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayotarajiwa kukutana mwishoni
mwa wiki.
0 comments:
Post a Comment