NJOMBE MJI YAJINASIBU KUPATA LIGI KUU BARA.



Uongozi wa timu ya Njombe Mji toka mkoa mpya wa Njombe umedhamiria kuutangaza mkoa huo kwa kutinga ligi kuu ya Tanzania bara kabla ya mwaka 2015.
Katibu wa Njombe mji Kaini Nyigu amesema hayo jioni ya jana baada ya kumaliza mchezo wa ligi ya mkoa dhidi ya Polisi Ludewa uliomalizika kwa timu ya Njombe mji kushinda magoli 8 kwa 2.
Kaini amesema  mafanikio hayo yametokana na maandalizi mazuri kabla ua kuanza kwa ligi ambapo walijihimu kucheza michezo mingi ikiwemo na timu ya taifa ya vijana Serengeti boys kwa lengo kujiimarisha zaidi.
Aliongeza kuwa lengo la klabu yao kurejesha heshima ya soka la nyanda za juu kusini iliyopotezwa na baadhi ya vilabu vikiwemo Lipuli, Tukuyu Stars pamoja na Nazaret ya Njombe.
Mwaka uliopita klabu hiyo ilishindwa kufanya vema wakati ikishiriki ligi kama klabu ya mkoa wa Iringa kitendo ambacho kaini amedai kushindwa kwao kumechangiwa na mizengwe ya uongozi wa soka mkoani Iringa.

0 comments:

Post a Comment