Siku chache baada ya uongozi wa Lipuli kupitia mwenyekiti
wakae Abnery Mrema kutangaza nia ya kuipandisha timu hiyo kongwe ya mkoa wa
Iringa kwa kuunda kamati ya fedha huku akiwataka wadau kujitokeza kuichangia
timu hiyo, mdau wa michezo ambayo pia ni mumbe wa NEC wa chama cha mapinduzi
Mh. Muimage Madenge ametanga kuiopanguvu timu hiyo yenye maskani yake wilaya ya
Iringa mjini.
Madenge amesema katika hatua yake ya kwanza atatoa kiasi cha
shilingi laki tano atakayokabidhi siku ya jumatatu ili kufananikisha mipango ya
awali ya klabu hiyo, huku akisisitiza kuwa ni wakati muafaka kwa wadau wa soka
Iringa kutazama timu hiyo iliyobeba jina kubwa lenye heshima duniani.
Siku moja iliyipita mwenyekiti wa Lipuli Abnery Mrema
alitangaza safu ya watu nane watakao simama katika kamati ya uhamasishaji wa
timu hiyo. Huku kamati hiyo ikiongozwa na mheshimiwa Rita Kabati kama
mwenyekiti wa kamati, Mhe, Ali Mbata katibu wa kamati huku wajumbe wakiwa ni Fredirick Mwakalebela,
Agostino Mrema,Haji Mwilu, Mohammed Msomali, Chuki Shabani pamoja na Husna
Mtasiwa.
Mrema amesisitiza kuwa walioteuliwa kwenye kamati hiyo
wamerdhia kuifanya kazi hiyo sambamba na kukubaliana na mkakati wa kupandisha
katika ligi kuu bara timu ya lipuli ifikapo mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment