Fainali
ya kombe la Mapinduzi imepigwa jana kwenye uwanja wa Amani kule Zanzibar ambapo
timu ya Azam imetwaa ubingwa wa michuano hiyo baada ya kupata ushindi wa magoli
2 kwa 1 dhidi ya Tusker ya kenya.
Katika
mchezo huo Tusker ilikuwa ya kwanza kufunga katika dakika ya 59 kupitia
mshambuliaji wake Jese Were, wakati magoli ya Azam yakifungwa na Jockins Atudo
kwa mkwaju wa Penati dakika 72 na Gaudience Mwaikimba 92.
Meneja
wa Azam FC, Patrick Kahemele amesema ushindi huo umeletwa na kujituma kwa
wachezaji wa klabu hiyo kuliko wapelekea kutoka kwenye kichapo cha goli moja
hadi kushinda magoli 2 kwa 1.
Kwa
matokeo hayo Azam imefikia rekodi ya Yanga ya mwaka 2004 na 2005 kwa kutwaa
taji hilo na kulitetea.
Kwa
upande mwingine Kahemelea amesema kuwa kikosi cha Azama kitasafiri mwishoni mwa
juma hili kuelekea Kenya kwaaajili ya michezo ya kirafiki ambayo ni sehemu ya
maandalizi ya ligi kuu na michezo ya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment