Licha ya kupoteza
mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya A.F.C Leopard, kocha wa Azam FC
Stewart Hall amesema timu yake imecheza vizuri na kufungwa ni sehemu ya mchezo.
Stewart alisema
haikuwa bahati kwao kwa kuwa walipata nafasi nyingi za wazi umaliziaji ukawa
tatizo, pia na penati mbili walizopata wachezaji wake walikosa na kuipa ushindi
timu hiyo ilikuwa na mashabiki wengi uwanjani hapo.
“Timu inayocheza
vizuri ni ile inayotengeneza nafasi na kucheza mpira mzuri, tulicheza vizuri
nafurahi kuona wachezaji wanajituma, kukosa penati na nafasi za wazi ni
matatizo yanaweza kuzibika” alisema Stewart
Aliongeza kuwa kupitia
mechi hizi zote watakuwa na wakati mzuri wa kurekebisha makosa yanayotokea
kabla ya kuanza kwa mechi za ligi.
Katika mchezo huo AFC
walikuwa wa kwanza kupata magoli yalifungwa katika dk ya 14 na Paul Were na dk
54 Mike Baraza aliifungia timu hiyo goli la pili kufuatia kosa la beki wa Azam
FC, David Mwantika kumruhusu akapiga shuti likaenda moja kwa moja wavuni.
Azam FC walipata
penati tatu katika dk 19, Jockins Atudo alikosa baada ya kupiga mkwaju uliotoka
nje, dk 65 Khamis Mcha nae alikosa penati baada ya kugonga mwamba na kurudi
ndani ikaokolewa na mabeki wa AFC.
Goli la Azam FC
lilipatikana kupitia kwa mkwaju wa penati iliyopigwa na Samih Haji Nuhu baada
ya beki wa AFC Erick Masika kumwangusha Humprey Mieno kwenye eneo la hatari.
Kipindi cha pili Kocha
Stewart alifanya mabadiliko walitoka, Luckson Kakolaki, Salum Abubakar,
Abdulhalim Humud, Uhuru Seleman, Jabir Aziz na Gaudence Mwaikimba nafasi zao
zikachukuliwa na David Mwantika, Michael Bolou,Humphrey Mieno, Ibrahim
Mwaipopo, Brian Umony na Abdi Kassim, mabadiliko hayo yaliimarisha kikosi hicho
muda wote wa mchezo
Baada ya mchezo huo
kocha wa AFC, Tom Olaba alisema kupata ushindi kwa kuifunga timu bora ni
mafanikio kwake na kuonyesha ukomavu kwa wachezaji wake.
“Unajua Azam FC ni
timu nzuri, tulijiandaa na kupanga kikosi ambacho kitapambana na timu hiyo,
nimefurahishwa na ushindi huo kwa kuwa nina wachezaji wapya saba katika timu
yangu na wamecheza vizuri na kushinda” alisema Olaba.
Azam FC leo Jumapili
jioni itacheza mechi ya pili dhidi ya SOFAPAKA kwenye Uwanja wa Nyayo jijini
Nairobi, kesho itapumzika na kufanya mazoezi katika Uwanja wa City kabla ya kucheza
na KCB katika Uwanja huo siku ya Jumanne.
Azam FC Mwadini Ally,
Himid Mao, Samih Haji Nuhu, Luckson Kakolaki/David Mwantika 45’, Jockins Atudo,
Jabir Aziz/Humphrey Mieno 45’, Salum Abubakar/Ibrahim Mwaipopo 45’, Abdulhalim
Humud/Michael Bolou 45’, Uhuru Seleman/Brain Umony 45’, Gaudence Mwaikimba/Abdi
Kassim 60’ na Khamis Mcha.
AFC Leopards Martin
Musaliya, Edwin Mafula, Noah Abichi, Erick Masika, Antony Kimani, Martin
Imbalambala/Michael Wendera, Benard Mangoli/Benard Ongoma, Patilah Omoto, Victor
Ochieng/Edward Seda, Mike Baraza/Noah Wafule na Paul Were
Mwisho
0 comments:
Post a Comment