Wadau watatu wa mpira wa miguu
wamechukua fomu za kuwania urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
na kufanya idadi ya waliojitosa katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24
mwaka huu kufikia 30.
Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa
wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana
kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz
ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18
mwaka huu.
Waliochukua leo (Januari 16 mwaka
huu) kuwania urais ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Jumanne
Nyamlani, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), Jamal
Emil Malinzi na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kigoma, Omari
Mussa Nkwarulo.
Mwengine aliyechukua leo ni
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias Mwanjala
anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuwakilisha Kanda ya Iringa na
Mbeya.
Orodha kamili ya wadau
waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil
Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais), Michael Wambura, Ramadhan Nassib na
Wallace Karia (umakamu wa rais).
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati
ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita),
Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na
Mwanza).
Epaphra Swai na Mbasha Matutu
(Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na Manyara),
Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na
Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi (Lindi na Mtwara),
Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi na Twahili
Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed
(Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder
(Dar es Salaam).
Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu
(TPL Board) waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf
Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania
umakamu mwenyekiti.
0 comments:
Post a Comment