
African Lyon ndiyo klabu
iliyoongoza kwa kusajili wachezaji wengi kwenye dirisha dogo kwa ajili ya
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom utakaotoa bingwa wa Tanzania Bara,
lakini pia timu tatu ambazo msimu ujao zitarudi kucheza Ligi Daraja la Kwanza.
Kati ya wachezaji 65
waliotua katika klabu mbalimbali katika dirisha hilo, Lyon ndiyo iliyoongoza
kwa kuwanasa 12. Miongoni mwao hao, wawili (Ibrahim Job na Shamte Ally)
imewachukua kwa mkopo kutoka Yanga.
Pia watano imewapandisha
kutoka katika kikosi chake cha U 20. Wachezaji hao ni Nurdin Musa, Salvatory
Jackson, Mohamed Athuman, Athuman Kajembe na jarufu Kizombi. Wengine walioingia
katika timu hiyo katika dirisha dogo ni Juma Seif (Huru), Buya Jamwaka (Burkina
Faso), Takang Valentine (Huru) na Yusuf Mgwao (Huru).
Nayo Polisi Morogoro katika
kuhakikisha inaondoka mkiani mwa ligi imesajili wachezaji wanane katika dirisha
dogo kama ilivyofanya Oljoro JKT ya Arusha.
Wachezaji wa kigeni
walioingia katika dirisha dogo ni Humphrey Mieno, Brian Umony, Jockins Atudo
(Azam), Donald Obimma na Ulugbe Chika (Toto Africans), Zuberi Hamis na Tinashe
Machemedze (Coastal Union), Musa Mudde na Abel Dhaila (Simba).
0 comments:
Post a Comment