Wakati kesho ndiyo mwisho wa
kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) waombaji
36 wameshachukua na 18 tayari wamesharejesha.
Waombaji wanne walioongezeka
katika orodha ni Blassy Kiondo kwa Kanda ya Katavi na Rukwa, Eliud Mvella
(Mbeya na Iringa), Geofrey Nyange (Morogoro na Pwani), na Omari Abdulkadir kwa
Kanda ya Dar es Salaam.
Orodha kamili ya waombaji ni
Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais) wakati waombaji
wa umakamu wa rais mpaka sasa ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace
Karia.
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati
ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita),
Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na
Mwanza).
Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga
na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo
(Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na
Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi na Zafarani Damoder
(Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid
Nahdi, Geofrey Nyange na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala na
Eliud Mvella (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin
Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).
Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu
(TPL Board) waliochukua fomu mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf Manji amechukua
fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu
mwenyekiti.
0 comments:
Post a Comment