WENGER AKIRI KUUMIZWA NA UKAME WA MATAJI.



 
Siku moja kabla ya kesho jumapili kucheza mchezo wa FA Cup dhidi ya Swansea kule Libery Stadium, Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Venga amekiri kuchanganyikiwa juu ya kukosa mataji akiwa na klabu yake ya Arsenal kwa miaka takribani nane sasa.
Venga amesema hayo wakati akizungumzia maandalizi ya mchezo wa raundi ya tatu ya michuano ya FA Cup dhidi ya Swansea ambapo amekiri kuona ukame wa mataji unaoendelea kwenye kikosi chake huku wakitazama vilabu vingine vikitwaa mataji tofauti.
Mfaransa huyo amesema anafikiri kuwa Arsenal ipo kwenye mwendo mzuri ila kiti kitakacho imarisha kikosi chake vizuri zaidi ni kutwaa taji la FA Cup ili kujenga imani ya washabiki kwenye klabu hiyo.
Desemba mwaka jana Arsenal iliondolewa kwenye robo fainali ya Capital One baada ya kufungwa na Bradford kwa mikwaju ya penati lakini sasa Wenger ameonesha nia ya kutaka kuindoa Swansea ambayo tayari iliifunga Arsenal magoli 2 kwa 0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya England.
Huu ni mwaka wa nane sasa Arsenal haijafanikiwa kutwaa kombe lolote huku mara ya mwisho Arsenal kufanya hivyo ni mwaka 2004 ilipotwaa taji la ligi kuu ya Englnd bila ya kufungwa hata mchezo mmoja.
MWISHO.

0 comments:

Post a Comment