RIJKAARD AFUNGISHWA VIRAGO



 
                             Rijkaard akiwa kazini SA.
Shirikisho la soka la Saudi Arabia SAFF limetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wa timu  ya soka ya taifa hilo raia wa Uholanzi Frank Rijkaard licha ya kuwa na mkataba wa miaka mitatu ya kuifundisha timu yao.
Rijkaard  wenye umri wa miaka 50 na aliyewahi kuifundisha Fc Barcelona  kuanzia mwaka 2003 hadi 2008 amesitishiwa  mkataba wake baada ya kushindwa kufanya vyema kwenye kombe la Gulf linaloshirikisha mataifa ya bara la Asia.
Shirikisho la soka nchini humo SAFF limebainisha kuwa limefikia makubaliano na kocha huyo juu ya kukatisha mkataba wake huku wakimshukuru kwa kazi aliyoifanya tangu achukue nafasi hiyo.
Nafasi ya Rijkaard aliyewahi kuzichezea timu za Ajax na AC Milan ya Italia imechukuliwa na makocha wawili Sergio Lopez Caro na  Salman Quraini ambao wataiongoza Saudi Arabia katika mechi za mchujo kwa kombe la dunia mwakani.

0 comments:

Post a Comment