Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Anna Makinda, ameombwa kuwasaidia mabondia wa mkoa wa Njombe kwa lengo la kuinua
mchezo wa ngumi katika mkoa huo mpya.
Hayo yamesemwa na raisi wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa
nchini TPBO Yasini Abdalaha Ustadh wakati akizungumza juu ya uwezo wa bondia wa
Njombe Chupak Chipindi.
Ustadh amesema si
vizuri kwa mkoa wa Njombe ambao umetoa muheshimiwa na spika wa bunge la
Tanzania lakini hakuna mchango wowote juu ya wanamasumbwi wa mkoa huo hukua
akisisitia kuwa fursa kubwa ya kuinua mchezo wa ngumi mkoani humo ipo kwa Spika
wa Bunge kwa sasa anapaswa kutazama zaidi mabondia wa mkoa huo.
Akimzungumzia Chupak Chipindi amesema Chupak ni bondia bora
na anahitaji kupata wawezeshaji ili kuweza kutangaza kipaji chake na autangaze
mkoa wa Njombe,
Chupak ni bondia wa uzito wa juu alikuwa akiwakilisha mkoa wa
Iringa hapo zamani kwa sasa Njombe mwishoni mwa mwaka 2012 alishindwa kwenda
nchini Hungary katika pambano la kimataifa huku moja vikwazo vilielezwa kuwa ni
ukata wa fedha.
0 comments:
Post a Comment