Uchaguzi wa
viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) utafanyika
Jumamosi (Januari 19 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Uhuru,
Dar es Salaam.
Kwa mujibu
wa Katibu Mkuu wa TAFCA, Eugene Mwasamaki, mikoa ambayo tayari imefanya
uchaguzi wa viongozi inatakiwa kuwasilisha muhtasari wa mkutano uliowaingiza
madarakani. Muhtasari huo uwasilishwe TAFCA kabla ya keshokutwa (Januari 17
mwaka huu).
Mkoa
utakaoshindwa kutuma muhtasari ndani ya muda uliotolewa utakosa haki ya
kushiriki katika uchaguzi huo uliovutia wagombea watano. Wagombea hao ni Oscar
Korosso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti), Michael Bundala
(Katibu Mkuu) na Magoma Rugora na Wilfred Kidao wanaowania ujumbe wa Mkutano
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
0 comments:
Post a Comment