
Timu ya Young Africans Sports Club kesho itashuka dimbani kucheza na timu ya Denizlispor FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uturuki katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika katika uwanja wa Selen Football -Kalimya Complex pembeni kidogo ya mji wa Antlaya.
Young Africans ambayo imeweka kambi ya
mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo huo kama fursa ya kujipima nguvu na timu
hiyo la Denizlispor FC ambayo imeshuka kutoka ligi kuu ya Uturuki mwaka
jana na hivi sasa inapamabana kurudi tena katika Ligi Kuu ya Uturuki.
Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest
Brandts amesema kwao ni furaha kupata nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya
Denizlispor FC ambayo ina wachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini
utakua ni mchezo safi na kuwavutia.
Baada ya kuwa na wiki moja ya mazoezi
na mechi moja ya kirafiki dhidi ya Armini Bielefeld ya ujerumani mwishoni mwa
wiki itakua ni fursa nyingine nzuri ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu
nyingine, hii itanisadia kuona maendeleo ya kikosi changu kutokana na mazoezi
ambayo tumekuwa tukiyafanya tangu tulipofika alisema 'Brandts'
Denizlispor FC ni miongoni mwa timu
zaidi ya 200 kutoka shemu tofauti duniani ambazo zimeweka kambi katika mji wa
Antlaya kwa ajili ya maandilizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la kwanza
nchini Uturuki.
Mchezaji wa zamani wa Leicester City ya
Uingereza, Dundee United ya Scotland na Ivernes ya Uholanzi, mtanzania mzaliwa
wa Uingereza Eric Odhiambo ni miongoni mwa washambuliaji wa kutegemewa wa timu
ya Denizlispor FC.
Young Africans imeendelea na mazoezi
katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo
utakaochezwa kesho katika uwanja wa Selen Football - Kalimya complex pemebeni
kidogo ya mji wa Antalya.
Kikosi cha wachezaji 27 waliopo mjini
Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna maheruhi hata mmoja hali
itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika mchezo huo.
Athumani Idd 'Chuji' na Hamis Kiiza
waliokuwa wakijisikia vibaya kabla ya mchezo wa juzi dhidi ya Amrnini Bielefeld
wanaendelea vizrui kabisa kwani wanaendelea na mazoezi pamoja na wachezaji
wengine waliopo na timu mjini Antalya.
Kuhusu hali ya hewa leo haijaonekana
kuwa tatizo kwa wachezaji kwani wanaonekana kuimudu na mda mwingi kwa sasa
kumekua na jua linalowaka kuanzia asubuhu wakati wa mazoezi mpaka mida ya
jioni, kwa leo hali ya hewa ni nyuzi joto 17 - 21, hivyo hali ya hewa ni nzuri
kabisa na jua linawaka mda wote.
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA YANGA.
0 comments:
Post a Comment