
Yanga iliyopiga kambi ya
mazoezi kwa takribani wiki mbili mjini Antalya, Uturuki itaanza mzunguko wa
pili dhidi ya Tanzania Prisons katika mechi itakayochezwa keshokutwa (Januari
27 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Vinara hao wa VPL wakiongoza
kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya Azam wanaowafuatia wanaikabili Tanzania
Prisons ambayo imetumia dirisha dogo kuongeza wachezaji wawili akiwemo
mshambuliaji mkongwe Emmanuel Gabriel.
Timu hizo zilitoka suluhu
katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,
jijini Mbeya. Hivyo kiu ya washabiki ni kutaka kujua nani ataibuka mbabe kati
ya timu hizo msimu huu.
Wakati ameingiza wachezaji
wawili kwenye dirisha dogo, Kocha wa Tanzania Prisons, Jumanne Chale amempoteza
David Mwantika katika dirisa hilo. Beki huyo ametua katika timu ya Azam.
0 comments:
Post a Comment