Mzunguko wa pili wa Ligi Daraja
la Kwanza (FDL) ambayo itatoa timu tatu zitakazocheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
msimu ujao (2013/2014) unaanza Jumamosi (Februari 2 mwaka huu) katika viwanja
tisa tofauti.
Kundi A litakuwa na mechi kati ya
Mbeya City na Burkina Faso itakayochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya,
Majimaji na Kurugenzi katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea, na Polisi Iringa
dhidi ya Mkamba Rangers kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa.
Mechi za Kundi B, Jumamosi
(Februari 2 mwaka huu) itakuwa Transit Camp na Ndanda itakayochezwa Uwanja wa
Mabatini mkoani Pwani, Moro United dhidi ya Villa Squad (Uwanja wa Karume, Dar
es Salaam). Jumapili (Februari 3 mwaka huu) ni Tessema na Green Warriors
(Mabatini, Pwani), Ashanti United na Polisi Dar (Uwanja wa Karume, Dar es
Salaam).
Kundi C Jumamosi (Februari 2
mwaka huu) ni Polisi Dodoma na Kanembwa JKT (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Morani
dhidi ya Mwadui (Uwanja wa Kiteto, Manyara), Polisi Mara na Pamba (Uwanja wa
Karume, Musoma), Polisi Tabora na Rhino Rangers (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,
Tabora).
0 comments:
Post a Comment