TFF KUBUKA NA HAYA KABLA NA BAADA YA UCHAGUZI.



 
Badaa ya kamati ya utendaji ya TFF,kukaa Novemba 3 mwaka huu yaliyopokelewa na kamati hiyo taarifa ya mapendekezo ya marekebisho ya Katiba TFF kama ifuatavyo:
1.    Kuingiza kipengele kinachohusu “Club Lincencing” kama ilivyoagizwa na CAF katika waraka wake unaowataka wanachama wote wa CAF, ikiwemo TFF, kuhakikisha kuwa kipengele hicho kinaingizwa katika katiba zao.
2.    Kutokana na ushauri na maagizo ya FIFA, TFF inatakiwa kuunda wa Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi (“Elections Appeals Committee”) na kuondokana na utaratibu tulionao hivi sasa ambao Kamati ya Rufaa (“Appeals Committee”) inajigeuza na kuwa Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi wakati wa mchakato wa uchaguzi wa TFF.
3.    Kuindoa nafasi ya Makamu wa Pili wa TFF pamoja na kutamka kuwa Wawakilishi wa klabu za Ligi Kuu katika Kamati ya Utendaji watachaguliwa moja kwa moja na klabu zenyewe. Hii inatokana na azimio la Mkutano Mkuu uliopita la kuruhusu uundwaji wa chombo huru cha kusimamia Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza pamoja na kupitishwa kwa Kanuni zinazokiongoza chombo hicho kama zilivyopendekezwa na klabu za Ligi Kuu na kupitishwa na Kamati ya Utendaji.
Baada ya kutafakari mapendekezo hayo, Kamati ya Utendaji ya TFF iliamua kuwa:
1.    Ipo haja ya kuifanyia marekebisho Katiba ya TFF kama iliyopendekezwa.
2.    Kwa vile mapendekezo mawili kati ya matatu ya marekebisho ya Katiba yana uhusiano na Uchaguzi Mkuu wa TFF, ipo haja ya marekebisho hayo kufanyika kabla ya kutangazwa kwa Mkutano Mkuu wa TFF na kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF.
3.    Aidha, kwa vile TFF haina uwezo wa kuitisha mikutano mikuu miwili – Mkutano Mkuu Maalum kwa ajili ya marekebisho ya Katiba ya TFF; na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi – katika kipindi kifupi kijacho, marekebisho ya Katiba yafanywe kwa njia ya Waraka (“Circular Resolution”).


0 comments:

Post a Comment