MVELA AWAONDOA HOFU WADAU JUU YA KESI YA RUSHWA.



              
                       Katibu wa IRFA Eliud Mvela.
Siku chache baada ya kupelekwa mahakani kwa tuhuma za rushwa katibu wa chama cha soka mkoani Iringa  Eliund Mvela amewataka wadau wa soka mkoani humo kuondoa hofu juu  ya kesi yake na kudai kuwa shughuri za soka zitaendelea kusonga kama kawaida kwa ushirikiano wake na wadau wa soka.
Akizungumza na mwananchi Mvella ambaye pia ni katibu wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka nchini Tanzania TFF amekataa kudhihirisha kama ni kweli alitoa rushwa ama hakutoa, kwa kusema kwa kuwa kesi ipo mahakani basi iachiwe mahakama kufanya maamuzi yake.
Mwishoni mwa juma lililopita Mvela alifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Mfawidhi kusomewa shitaka linalomkabili la rushwa ambapo kamanda wa TAKUKURU Mkoani iringa Emma Kuhanga alithibitisha kuwa Mvela ameshtakiwa lwa kifungu cha 15. 1b kifungu cha sheria namba 11 cha mwaka 2007.
katika taarifa yake Kuhanga alisema mnamo tarehe 27 Septemba 2012 katika maeneo ya Kihesa Ngome, mtuhumiwa akiwa mgombea wa CCM alimpa Katibu wa chama hicho Kata ya Kihesa Yusuph Mabena shilingi elfu 70 ambayo igawanywe kwa wana CCM waliokuwa wamekusanyika katika nyumba ya Anna Myinga ikiwa kama kishawishi kwao ili waweze kumpigia kura katika nafasi aliyokuwa akigombea.

mbali na harakati hizo  za utoaji rushwa katika uchaguzi wa CCM mkoa uliofanyika Septemba 28, mwaka huu, Mvela alikuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa wilaya hakufanikiwa kushinda kutokana na kuandamwa kwa rushwa.
 Kwa mujibu wa kifungu hicho, Mtuhumiwa wa makosa kama hayo endapo atashindwa kesi atatakiwa kulipa faini kati ya shilingi laki tano na milioni moja au kutumikia jela kati ya muda wa miaka isiyopungua 3 na isiyozidi 5.
 Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa ambapo itaanza kusikilizwa Desemba 13, mwaka huu.
kutokana na kesi hiyo wadau waliowengi wamekuwa na shaka ikiwemo kuondoa imani ya kiongozi wao wa soka ambaye anadhima kubwa ya kiutendaji katika soka la Iringa.
 

0 comments:

Post a Comment