RAS wa mkoa
wa Iringa, Mheshimiwa Getrude Mpaka, ameitaka wizara ya fedha kuzitazama timu
za mikoa na idara mbalimbali za serikali katika kuziwezesha kifedha ilikuziweka
katika hali nzuri kimashindano kama zilivyo timu za wizara mbalimbali.
Mpaka amesema
hayo katika hafla fupi ya kukabidhiwa zawadi ya mshindi wa pili iliyoletwa na
timu ya kuvuta Kamba kwa wanawake toka mkoani Iringa.
Katika hafla
hiyo iliyofanyika ofisini kwake Mpaka amesema ni dhahiri kwamba wanashindwa
kushiriki michezo mingi katika michuano ya Shimiwi kutokana na uhaba wa fedha
za maandalizi na tofauti na timu za wizara ya fedha na nyinginezo wana mudu
kushiriki takribani michezo yote kutokana na kuwa na fedha za kutosha za
maandalizi.
Kwa upande
mwingine Mpaka amewataka wanamichezo hao wa Serikali ya mkoa wa Iringa kufanya
mazoezi kila kukicha ili kuboresha vikosi vyao kwaajili ya michuano mbalimbali.
Naye nadhoa
wa timu ya kuvuta Kamba mkoani humo Agness Mlula amemshukuru Mh.Mpaka kwa
ushirikiano alioutoa hadi kufikia mafanikio huku akisisitiza juu ya serikali
kuu kuziangalia timu hizo ziweze kufanya vema kwenye michezo.
Michuano ya
SHIMIWI kwa mwaka 2012 ilifanyika mkoani Morogoro ambapo ilianza Sepetemba 22 na kumalizika Oktoba 6 huku timu ya Ras Iringa ikitoka na zawadi ya
kikombe baada ya kuvutwa na timu ya Ikulu waliyokutana nayo kwenye mchezo wa
fainali.
0 comments:
Post a Comment