HAYATOU KUFUNGUA CECAFA.



                 
                                     Rais wa CAF Issa Hayatou.
Baraza la vyama vya Soka Afrika mashariki CECAFA na shirikisho la soka la nchini Uganda nd FUFA alimethibitisha kuwa raisi wa CAF Issa Hayatou atakuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya ufunguzi wa michuano ya CECAFA Challenge Cup inayotaraji kuanza hivi karibu Novemba 24 mwaka kule nchini Uganda.
Akithibitisha hilo msemaji wa FUFA na CECAFA Rodgers Mulindwa amesema tayari mipango imekalika na Hayatou atawasili nchini Uganda Novemba 22 na kuhudhuria kwenye haflaya ufunguzi huku akipokewa na raisi wa CECAFA Leodga Chila Tenga.
Kwa upande wake raisi wa FUFA Lawrence Mulindwa amesema ni heshima kubwa kwa Uganda kuandaa michuano hiyo lakini pia ni nguvu ya kutosha katika kukuza endapo Hayatou atashiriki kwenye michuano hiyo mikubwa ya ukandahuu wa CECAFA..
Katika michuano hiyo Novemba 24 Uganda itafungua dimba na Kenya kwenye mchezo mkubwa Ufunguzi wakati Tanzania bara itacheza Nove 25 na Sudan.

0 comments:

Post a Comment