
Mbunge wa
jimbo la Iringa mjini Mch. Peter Msigwa ameandaa michuano mikubwa wilayani humo
itakayoshirikisha takribani vilabu 28 vya jimboni mwake.
Akizungumza
na blog hii, mratibu wa michezo kwenye ofisi ya mbunge huyo Abu Changawa
amesema michuano hiyo itakayochezwa kwa mtindo wa makundi ambayo yatatoka kila
kanda ya jimbo hilo inataraji kuanza Nov 26 mwaka huu na imegharimu kiasi cha shilingi milion kumi na
nane na laki tano za kitanzania (18,500,000/=) kwa maandalizi ya vitu vyote vya
mashindano mpaka zawadi za michuano hiyo.
Changawa amesema
kabla ya kuanza kwa michuano hiyo kilatimu itapewa jezi kwaajili ya maandalizi
ya kushiriki michuano hiyo, na kwa upande wa zawadi bingwa michuano hiyo atapa kitita cha shilingi
milioni moja, mshindi wa pili shilingi laki saba wakati mshindi wa tatu
atachukua kiasi cha shili laki tano, mbali na zawadi hizo kutakuwa na zawadi za
timu yenye nidhamu, mfungaji bora, kipa bora pamoja na mwamuzi bora ambao wote
watapata zawadi ya shilingi laki moja moja.
Wakati huo
huuo Mch. Msigwa hakuwasahau waandishi wa michezo baada ya kutenga zawadi ya
shilingi laki tatu kwa mwandishi bora wa gazeti, redio, na TV wakati mshindi wa pili tasnia hii ya habari wakipangwa kuchukua kiasi
cha shilingi mbili kwa kila Nyanja.
Mwanzoni mwa
mwezi uliopita Mheshimiwa Mch. Msigwa alikilaumu chama cha soka cha wilaya ya
Iringa mjini IMDFA kwa kumnyima nafasi ya kudhamini ligi ya wilaya hiyo kwa
madai kuwa wameiingiza siasakwenye mchezo wa soka na sasa ligi hiyo
inadhaminiwa na Fredilick Mwakalebela.
0 comments:
Post a Comment