
Mbembe kushoto akiwa na katibu wa Azam Nassor Idrissa na kocha msaidizi Kally Ongala.
Azam
FC inatangaza msiba wa mchua misuli (Masseur) wake Khamis Mbembe uliotokea leo
saa tano asubuhi... Khamis Mbembe alikuwa mcheshi, muungwana na mchapakazi
hodari ambaye anatuachia pengo kubwa sana klabuni.
Mbembe alipata maradhi
Mbembe alipata maradhi
ya kupooza yaliyomsumbua
kwa kipindi kirefu taratibu tangia June mwaka jana ambapo alipumzika kufanya
kazi Azam FC Novemba mwaka jana ili kupata matibabu zaidi ambapo Klabu ya Azam
FC na familia ya Mbembe kwa pamoja tulihangaika bila mafanikio. mwenyezi mungu
alitoa na yeye ndiye aliyetwaa... Tunamuombea dua marehemu roho yake ipumzike
mahala pema peponi. Amin
pichani
Mbembe kushoto mwenye ndevu na koti jeusi akiwa na Katibu mkuu wa Azam FC
Nassor Idrissa na kocha msaidizi Kally Ongala nchini Rwanda
Chanzo Azam Web.
Chanzo Azam Web.
0 comments:
Post a Comment