DI MATEO NJE CHELSEA



                      File:Dimatteo2 cropped.jpg
Uongozi wa klabu ya Chelsea umemfukuza kazi menejea wake Roberto Di Matteo baada ya kuitumikia klabu hiyo takribani kwa miezi minane na kuipatia mataji mawili ya FA Cup na ligi ya mabingwa barani ulaya.
Kwamujibu wa taarifa toka kwenye mtandao wa klabu hiyo Di Mateo amefukuzwa kazi baada ya kikao cha bodi na mmiliki wa klabu hiyo na kilicho jadili hatma ya meneja huyo na kutoridhika na utendaji wake haswa kwa matokeo ya hivi karibuni.
Bodi hiyo imemshukuru  Di Mateo kwa alichokifanya kwa kipindi chote haswa kuleta taji kubwa barani ulaya la ligi ya mabingwa alipoifunga Bayern Munich kwenye  mchezo wa fainali mei 19 mwaka huu.
Matokeo mabaya ya ligi ya mabingwa yaliyopoteza matumaini ya kutetea ubingwa wa ulaya na yale ligi kuu ya England yaliyoitoa timu hiyo kileleni hadi nafasi ya tatu yameonekana kuwa chanzo mbali na kucheza soka la kuvutia linalotakiwa na mmiliki wa klabu hiyo.
Di Mateo mwenye umri wa miaka  42 aliwahi kuichezea timu hiyo kuanzia mwaka 1996 hadi 2002 na juni 13 mwaka huu alipewa mkataba wa miaka miwili kama meneja wa timu hiyo baada ya kukaimu vema nafasi ya aliekuwa kocha wa timu hiyo Andres Vila Boas.
MWISHO.
Mameneja waliopita tangu Roman Abramovich ainunue Chelsea.
  • Claudio Ranieri: Sep 2000 to May 2004
  • Jose Mourinho: Jun 2004 to Sep 2007
  • Avram Grant: Sep 2007 to May 2008
  • Luiz Felipe Scolari: Jul 2008 to Feb 2009
  • Guus Hiddink: Feb 2009 to May 2009
  • Carlo Ancelotti: Jun 2009 to May 2011
  • Andre Villas-Boas: Jun 2011 to Mar 2012
  • Roberto Di Matteo: Mar 2012 to Nov 2012

0 comments:

Post a Comment