MUDIFA YA AONGEZA SIKU YA KURJESHA FOMU.



Chama cha soka wilayani Mufindi umeongeza siku moja ya kukusanya fomu za usajili wa vilabu vilivyoshindwa kufikisha fomu  za usajili wa wachezaji kwa wakati katika ofisi za chama hicho.

Katibu wa MUDIFA Festor Kilipamwambu amesema tarehe ya mwisho ya kurejesha fomu hizo ni leo lakini mpaka sasa vilabu 12 vimerejesha na takribani vilabu vitano havija rejesha fomu hizo ndio maana wamefikia maamuzi ya kuongeza siku hadi Novemba 21 kwaajili ya kurejesha fomu hizo.

kwa upande mwingine Kilipamwambu amesema kuwa siku ya Alhmisi watakuwa na kikao na viongozi wote wa vilabu ili kuzungumzia mustakbali wa ligi na ratiba ya ligi hiyo.

0 comments:

Post a Comment