
Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya England, David Beckham anataraji kuondoka kwenye klabu yake ya Los
Angeles Galaxy ya nchini Marekani, mwezi ujao mara baada ya kumaliza kucheza
fainali ya michuano ya MLS Cup itakayofanyika Desemba mosi mwa huu.
Beckam
mwenye umri wa miaka 37 sasa amesema mchezo wa fainali dhidi ya Hoston Dynamo
utakuwa mchezo wake wa mwisho akiwa na La Galaxy baada ya kutumikia klabu hiyo
kwa takribani miaka sita sasa.Aidha Beckam aliyejijengea historia kubwa mnamo 1999 alipotwaa mataji mfululizo akiwa na Manchester United, amesema anataka kuingia katika changamoto nyingine ya mchezo wa soka kabla ya kufunga milango ya kulitumikia soka ulimwenguni.
Wakati huohuo mkurugenzi wa klabu ya Melbourne Heart nchini Australia, Scott Munn, amesema kuwa wanahitaji kufanya kazi nyota wa zamani wa Manchester united huku akithibisha kuwa wapo katika mazungumzo yatakayo malizika hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment