BENITZ AINGIA KWENYE KIKOSI CHA MAJANGILI.



 Rafael Benitez
    Huyu ndiye Benitez aliyekabidhiwa mfupa uliyemshinda Fisi.
Masaa kadhaa baada ya kumfukuza aliyekuwa kocha wake Roberto Di Matteo uongozi wa klabu ya Chelsea umemteua kocha wa zamani wa klabu ya Liverpool Rafael Banitez kuziba nafasi hiyo hadi mwishoni mwa msimu huu.
Benitez mwenye umri wa miaka 52 mara baada ya kutangazwa kuchukua nafasi hiyo anatarajiwa kukutana na mmiliki wa Chelsea Roman Abromovich ilikumalizana naye katika baadhi ya mambo mhimu.
Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye mtandano wa klabu hiyo imeeleza kuwa mmliki wamabingwa hao wa ulaya kwa upande wa vilabu na bodi ya wakurugenzi wanaimani kuwa Benitez ni chaguo sahihi kwakuwa anauzoefu wa kutosha.
Benitez aliyefukuzwa na Inter Milan december mwaka 2010 baada ya kuifundisha timu hiyo kwa miezi sita anatarajiwa kuhudhuria mazoezi ya timu yake mpya leo.
Benitez anakuwa kocha wa 9 kushika nafasi hiyo ndani ya klabu ya chelsea tangu inunuliwe na bilionea huyo raia wa Urusi mnamo mwaka 2003.

0 comments:

Post a Comment