TANDAU AISHUKIA TFF JUU YA MAPATO.



Kamati ya saidia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys imeshangazwa na utaratibu wa makato ya fedha zilizopatikana mara baada ya mashabiki kujitokeza katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam wakati wa mchezo wa kwanza kati ya timu hiyo dhidi ya timu ya taifa ya Kongo Brazzaville uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Katibu wa kamati hiyo Henry Tandau amesema makato ya fedha zilizopatikana yamewashangaza kutokana na dhana ya utaifa kuwekwa nyuma na badala yake kuiacha kamati yao na harakati nzito za kuendelea kuisaidia Serengeti boys.

Msikilize Tandau akiishukia TFF juu ya mapato

0 comments:

Post a Comment