BABA WA NGASA AFUNGUKA KUHUSU MWANAE.



Moja kati ya matuki ya makubwa ya Ngasa katika soka.
 Baba mzazi wa mshambuliaji wa Simba Mrisho Ngasa ambaye kwa sasa ni kocha wa  klabu ya Polisi Iringa na Khalfani Ngasa amefunguka juu ya kutotazamwa vizuri na mwanae katika mambo mbalimbali yanayomuhusu katika maisha yake.
Akizungumza na Mwananchi Ngasa amesema yanayozungumzwa kuhusu mtoto wake si yakweli na anamtimizia kila anachokitaka. “Ngasa ni mwanangu nashukuru naishi naye vizuri ananiheshimu nami na muheshimu, hajawahi kunitolea hata neno moja la kijeuri tangu pale alipoanza kupata jina katika medani ya soka na kuhusu msaada ananisaidia pale kwa wakati bila ya matatizo yoyote” Mzee Ngasa alisema hivyo.
Aidha mzee Ngasa amekana kauli za wadau wanaodai kuwa Mrisho ameshuka kiwango kutokana na kuwa na wake watatu kama inavyoruhusiwa imani yake ya kiislamu, amesema si kweli Ngasa hana wake wa tatu zidi ya mmoja aliemuoa miaka michache iliyopita na hajakubaliana na suala kushuka kiwangp cha mwanae huku akisema kwamba mchezo wa soka unaendana na sera ya timu kwa hiyo nivugumu kwa mchezaji kukopi iana timu mapema mno.
Kuhusu kipaji cha Ngasa amesema yeye alitarajia kuwa mtoto wake angefika hapa alipo sasa kutokana alipita katika mikono yake akiwa kama kocha,kwenye kituo maarufu cha soka  cha Channel Africa,kilichopo jijini Mwanza wilaya ya Ilemelea, akiwemo ngasa na nyota wengine kama Henry Joseph aliopo Sweden akicheza soka la kulipwa.

0 comments:

Post a Comment