IVO MAPUNDA AIPELEKA GOR MAHIA FAINALI.



    
Mabingwa watetezi wa michuano ya FKF CUP ya nchini Kenya Gormahia  jioni ya leo wamefanya makubwa baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2 kwa 1dhidi ya AFC Leopards.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Moi International uliopo katika mji Kasarani mlinda mlango wa Tanzania Ivo Mapunda aliibuka kuwa shujaa mkubwa baada yakutoa pasi ndefu iliyosababisha goli la kwanza lililofungwa na Kevin Omondi katika dakika ya 12. Wakati goli la pili likifungwa na nyota wa zamani wa Simba na Yanga ambaye ni nahodha wa Gormahia Moses Odhiambo alifunga goli hilo katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
Kwa matokeo hayo Gormahia inasubiri kucheza fainali na mshindi kati ya Tusker na Sofapaka watakaocheza nusu fainali ya michuano hiyo.

0 comments:

Post a Comment