
Timu ya Los Angeles Lakers hapo jana ilikumbana na kichapo cha pili cha vikapu 116 na 106 dtoka kwa vijana wa Trail Blazers PORTLAND, katika mchezo wake wa pili wa ligi ya NBA.
Mbali na kupoteza mchezo huo klabu ya Lakers imepata pigo kubwa baada ya nyota wake Steve Nash kupata jeraha baada ya kugongwa na Damian Lillard wa Portland huku Dwight Howard akitolewa kwenye mchezo kwa majeraha.
Akizungumzia hilo kocha wa Lakers mara baada ya mchezo, Mikel Brown hii leo amesema kuwa hawezi kuzungumza chochote juu ya maumivu Nash huku akibaki na maumaini ya kumtumia mchezaji huyo kwenye mchezo wa Ijumaa dhidi ya Los Angeles Clippers.
Mara ya mwisho wa timu ya Lakers kutwaa taji la ligi ya NBA ni mwaka 2012 chini ya kocha Phil Jackson ambapo Lakers iliifunga Boston Celtics katika michezo minne kati ya michezo saba.
0 comments:
Post a Comment