Shujaa alieipandisha Lipuli mwa 1991 Chachage Bukaza.
Nyota wa zamani wa timu ya Lipuli ya Iringa Dr.Chachage
Bukaza kutokuwepo kwa nguvu ya makampuni yanayomiliki na kusimamia vilabu soka
la Iringa haliwezi kusimama kwenye mstari wa zamani wa ushindani katika soka.
Bukaza ambaye kwa sasa na muhadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini
kilichopo mkoani Iringa huku akiwa na historia kubwa ya soka mkoani Iringa
ambapo mwaka 1991 Chacha alifunga goli pekee lililo iwezesha Lipuli kupanda kwa
mara ya kwanza ligi kuu ya Tanzania bara.
Amesema tatizo kubwa la kudumaa kwa soka mkoani Iringa ni
kukosekana kwa fedha na watu wakutazama mchezo huku akielezea kipindi cha nyuma
wao walikuwa wakifanya makubwa kutokana walikuwa wakitazamwa na kupata kila
wanacho kihitaji katika timu zao.
Aliongeza pia kuwepo kwa timu za Retco, Pareto, Chai na
makampuni kulichangia kuwepo kwa mafanikio ya soka kwa wakati huo.
Wakati huo huyo katibu wa chama cha soka mkoani Iringa Eliud
Mvela amesema lazima wadau watoboe mifuko yao kuchangia soka ikiwemo timu ya
Polisi Iringa ambayo kwa sasa inawania nafasi ya kupanda ligi kuu ya Tanzania
bara, amesema wadau wapo wengi ila ni viongozi wa lawama kuliko kuchangia na
kutaka kutambua hali ya vilabu vinavyowakilisha mkoa.
Soka la Iringa limepotea kwenye ramani ya kitaifa kwa maana
ya ligi kuu ya Tanzania bara tangu mwaka 1999 iliposhuka daraja kutoka ligi kuu
ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment