OKWI AFUNGA MIDIMO YA WANAJANGWANI.


Mshambuliaji Emmanuel Okwi amewasili jijini Dar Es Salaam hii leo tayari kwa ajili ya siku ya Simba ya hapo kesho,
Kwamujibu wa msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga amenihakikishia ya kwamba Okwi yupo mjini na wakati naongea naye alikuwa klabuni mtaa wa Msimbazi akijiandaa kwenda viwanja vya TCC Chang'ombe kwa ajili ya Mazoezi.

Ujio wa Okwi umezima ndoto za mashabiki wengi wa Simba walitokwa na imani ya kuendelea kumtumia mchezaji huyo msimu huu huku mashabiki wa Yanga wakiwa na imani kuwa huenda akajiunga na klabu yao ya jangwani.

CHOMBO AFUNGUKA JUU YA MKATABA WAKE NA SIMBA


Aliyekuwa mchezaji wa Azam Fc Ramadhani Chombo Ridondoo leo ameweka wazi kuhusu mkataba wake mpya aliosaini jana kuchezea simba msimu huu.

Chombo amesema mkataba wake na Azam umemalizika mwezi juni mwaka huu na alikuwa na ugomvi mkubwa na klabu hiyo ambapo alifungiwa kwa muda wa miezi minne bila kulipwa mshahara .

Amesema amesugua benchi kusubiri mkataba mwingine lakini hakukuwa na hata kiongozi wa kumuongeza matokeo akasaini na Simba.

Hapo jana kiungo huyo wa kitanzania mwenye sifa ya kufanya vitu vya ajabu akiwa uwanjani alisaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Simba kwa dau la shilingi milioni 30.

BOCA AULA AZAM KUMRITH HALL.


Hii ni kali ya leo siku chache baada ya kocha mkuu wa klabu ya Azam Stewart Jonh Hall kutimuliwa kazi na klabu yake ya Azam hii leo klabu ya Azam imetangaza kumuajili kocha mpya wa klabu hiyo Boris Bunjak raia wa Serbia.

Kocha anasifika kwa uzoefu wa miaka zaidi ya kumi kati ufundishaji wa soka huku akiiingia katika nchi ambayo tayari makocha takriani saba wa Kiserbia wa kiwa wameshawasili kufundisha soka.

CV yakocha huyo ni.

BORIS BUNJAK

Born :
 17.11.1954.
Nationality :Serbian
Position :Coach
Languages :English , Rusian , Serbian
Current address :Kraljevo 36000 Veljka Vlahovica 33/15
Serbia
Contact :Serbian mob : +38163 776 44 88
Home number + fax : +38136 322 735
E-mail : bbunjak@yahoo.com
Facebook : Boris Bunjak
www.borisbunjakcoach.com
Education :Higher coach of football
UEFA – PRO LICENCE
Coaching career :2011         FC „DAMAC“ SAUDI ARABIA- HEAD COACH     
2011-       gd-jpeg v1.0 (using IJG JPEG v62), quality = 95  FC „ AL NASER“ OMAN – HEAD COACH
2009-10     FC „ AL OROUBA“ OMAN – HEAD COACH
2008-09      FC „ ALL SHAAB“ UNITED ARAB EMIRATES –  
                        TECHNICAL  SUPERVISOR
2007-08      FC „ ALL SHAAB“ UNITED ARAB EMIRATES – HEAD
                             COACH
2006-07      FC „ AL NASER“ OMAN – HEAD COACH
2005-06      FKHAJDUK“ Kula – HEAD COACH
2004-05      FC „ALL SHAAB“ UNITED ARAB EMIRATES – FIRST
                        TEAMCOACH
2002-04  FK „CRVENA ZVEZDA“ BeogradFIRST TEAM COACH
2000-02    FKMLADI RADNIK“ Pozarevac - HEAD COACH
1999-00     FKURALAN“ Russia - HEAD COACH
1998-99     FKRADNICKI“ Nis - HEAD COACH
1996-97    FKCRVENA ZVEZDA“ Gnjilane - HEAD COACH
1995-96     FK „JAVOR“ Ivanjica -  HEAD COACH    
1993-94     INSTRUCTOR IN FA of Yugoslavia
1990-93    FK „ SLOGA“ Kraljevo – HEAD COACH    
Playing career :     
 1967-75  FK „SLOGA“ Kraljevo
 1975-78  FK „VOZDOVAC“ Beograd
 1978-79  FK „RADNICKI“ Kragujevac
 1979-80  FK „ OLIMPIA“ Ljubljana
 1980-81  FK „ SUMADIJA“ Arandjelovac
 1981-85  FK „SLOGA“ Kraljevo
 1985-86  FK „BORAC“ Cacak
 1986-90  FK „ SLOGA“ Kraljevo

HII NI KAULI YA JAPHA IDDI WA AZAM KWA MAUZO YA CHOMBO SIMBA.

 
Simba SC imejichanganya kumsajili mchezaji  Ramadhani Suleiman Chombo ‘Redondo’, bila kuwasiliana na klabu yake na yatawatokea kama yaliyowatokea kwa Ibrahim Rajab ‘Jeba’, kupoteza fedha zao walizompa mchezaji.
 
haya yamesemwa na Japha Iddi hii leo wakati akizungumzia suala la usajili uliofanywa na Simba kwa kiungo wake Ramadhani Chombo.

TENGA KUZINDUA SEMINA YA UTAWALA.

                                                              Raisi wa TFFM Tenga

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) anatarajia kufungua Kozi ya Uongozi na Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayoanza kesho (Agosti 6 mwaka huu) Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.
 
Kozi hiyo itakayokuwa na washiriki zaidi ya 30 itamalizika Agosti 11 mwaka huu na itaendeshwa na Wakufunzi kutoka FIFA na itafunguliwa saa 3 asubuhi. Wakufunzi hao ni Barry Rukoro anayetoka Namibia, Henry Tandau (Tanzania) na Senka Kanyenvu (Botswana).
 
Baadhi ya washiriki wa kozi hiyo ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, Rais wa ZFA Amani Makungu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Ahmed Mgoyi, Blassy Kiondo, Stanley Lugenge, Khalid Abdallah, Hussein Mwamba na Eliud Mvella.
 
Wengine ni Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Salum, Katibu Msaidizi wa ZFA, Masoud Attai, wenyeviti wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal Malinzi), Dodoma (Nassoro Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).
 
Makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Mara (Mugisha Galibona), Mtwara (Vincent Majiri), Morogoro (Hamisi Semka), Kagera (Salum Chama), Tanga (Beatrice Mgaya) na Dodoma (Stuart Masima). Pia yumo Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Hilal na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.
 
Washiriki wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni, Ofisa Habari, Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na Matukio, Jimmy Kabwe na Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba.
 
Wengine ni Ofisa Sheria wa TFF, Neema Lucumay, Ofisa wa Mpira wa Miguu wa Wanawake, Grace Buretha, Amina Karuma (Mpira wa miguu wa wanawake) na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.

CHEKA AZIDI KUTIKISA


Shirikisho la Ngumi za Kulipwa na Chama cha ngumi Cha Marekani (IBF/USBA) kipo katika mchakato wa kuidhinisha pamnbano la ubingwa wa mabara katia ya bingwa wa IBF katika bara la Arika Francis Cheka na bingwa anayeshikilia ubingwa wa mabara Benjamim Simon wa Ujerumani.

Nafasi ya Francis Cheka inakuja baada ya kutamba kwenye orodha ya viwango vya abara vya IBF tola mwaka 2011 kama ifuatavyo:

January 2011: Alikuwa kwenye namba 15

February 2011: Alikuwa kwenye namba 14

March 2011: Alikuwa kwenye namba 14

April 2012: Alikuwa kwenye namba 13

May 2012: Alikuwa kwenye namba 13

June 2012: Alikuwa kwenye namba 12

July 2012: Alikuwa kwenye namba 11

August 2011: Alikuwa kwenye namba 10

September 2011: Alikuwa kwenye namba 7

October 2011: Alikuwa kwenye namba 5

November 2012: Alikuwa kwenye namba 6

December 2011: Alikuwa kwenye namba 6

January 2012: Alikuwa kwenye namba 6

February 2012: Alikuwa kwenye namba 6

March 2012: Alikuwa kwenye namba 5

ALIHAMIA UZITO WA SUPER MIDDLEWEIGHT BAADA YA KUWA BINGWA WA IBF AFRICA

April 2012: Alikuwa kwenye namba 5

May 2012: Alikuwa kwenye namba 14

June 2012: Alikuwa kwenye namba 15

July 2012: Yuko kwenye namba 15

Licha kwa taarifa za uongo zilizotolewa n Issac Gamba kwenye kipindi cha Radio One (ambacho hata hivyo Radio One hawakutaka kunitafuta wakati wakijua kuwa mimi ndiye mkuu wa IBF hapa Afrika)  kwamba Francis Cheka hatambuliki na IBF mpambano huo unakuja wakati tayari watu wenye tamaa za kama fisi wameshachungulia dili na kuanza kutoa taarifa za uongo ili waambiwe kuwa wao ndio wametafuta pambano hili.

Njaa na tamaa hizo zitaliharibia taifa hili heshima kubwa kwani watu hao wanadai kuwa wanafanya hayo kwa msukumo wa Wizara ya Habari na Michezo  Ikuguatana na kipindi hicho kkilivhorushwa na rdio One leo tarehe 4 Agosti siku ya Jumamosi saa moja na dakika arobaini na mbili usiku kikirushwa na Issac Gamba akimhoji Emmanauel Mlundwa).

Mpambano huo wa Ujerumani unaandaliwa na Promota Eva Rolle ambaye ni mdau mkuu wa IBF nchini Ujerumani. Wote tulishiriki kwemney mmktano mkuu wa IBF/USBA katika jiji la Honolulu mwaka huu kuanzia tarehe 28 may hadi 3 June 2012. Cheka akishinda mpambano huu ataingia kwenye viwango vya dunia na hivyo kumweka kwenye nafasi nzuri ya kucheza ubingwa wa dunia.

Napenda kuwashauri waandishi wote wanaotaka kupata habari sahihi kuhusu IBF hapa Afrika na mahali pengine popote duniani wawasiliane na mimi kwa kutumia simu namba 0754-360828 au barua pepe ngowio@yahoo.com .

Mimi ndiye kiongozi MKUU wa IBF/USBA katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi. Hivyo kama kweli unataka kupata habari sahihi za IBF na sio za uongo wa kutunga naomba tuwasiliane kwa simu pamoja na barua pepe hiyo hapo juu!
Taarifa hii Imetolewa na:



Onesmo A.M. Ngowi

Rais, Shirikisho la Ngumi la Kimataifa

Bara la Afrika, mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi

FAINALI YA SATETA YA LALA.

Fainali ya kombe la Politani Cup imelazwa hii leo na kusuburi tarahe nyingine baada ya mchezo huo uliowakutanisha Wangongo na Sateta kumalizika kwa sare ya magoli mawili kwa mawili.

Katika mchezo huo Wangongo walikuwa wakwanza kufunga baada ya mshambuliaji wake Nassor Saidi maarufu kama Choro kufunga goli kwa faulo yenye ufundi wa hali ya juu, hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Wangongo walikuwa wababe wa Sateta.

Katika dakika za mwisho za mchezo huo timu ya Sateta ilimudu kuchomoa goli hilo kupitia Amos Mgisa na baadae kufunga goli la pili lilifungwa na Adam Kingwande na kufunika matumaini ya mashabiki wa Wangongo waliokuwa na uchu wakutaka kufuturu wakiwa mabingwa wa kombe hilo.

Dakika sita baadaye Sateta walipachika goli la 2 na kusawazisha kwa kuweka sare ya magoli mawili kwa mawili.

Dakika tano baadaye mwamuzi Omary alimaliza mchezo huo na kupatika maamuzi ya kuahilishwa kwa pambano na waandaji wa pambano kitendo ambacho hakikupendwa na mashabiki wengi.

Kwa mujibu wa waandaji wa mashindano hayo imeelezwa kuwa mchezo huo huenda ukarudiwa jumapili ijayo baada ya mazungumzo na timu zote mbili.

YANGA YAENDA DODOMA.

                               Yanga ilivyotinga bungeni mwaka 2011 baada ya kutwaa ubingwa.

Klabu ya soka ya Yanga imesafiri mchana wa leo kulekea mjini Dodoma tayari kwa kuringisha kombe lake la Kagame ambalo wamelitetea kwa mara ya pili na kulibakisha nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa msemaji wa Yanga Luis Sendeu amaesema baada ya ziara hiyo Yanga itarejea Dar kwa maandalizi zaidi ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Hapo jana klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi mshambuliaji wake mpya Didier Kavumbagu aliesajiliwa na mabingwa hao wa Kagame julai 28 mwaka huu akitokea klabu ya Atretico ya Burundi.

SATETA KUUUMANA NA WANGONGO KWENYE MCHEZO WA FAINALI.

Kimetimuka kwenye uwanja wa Bandari wilayani Temeke jijini Dar es Salaam kwa mchezo wa fainali ya kombe la Ng`ombe kwa mchezo kati ya Ajax Mzamba maarufu kama Wangongo wakicheza na Sateta FC zote za Temeke.

Ni ngoma ambayo imetawaliwa na mastaa wengi wa ligi kuu ya Tanzania bara akiwemo Amos wa JKT Ruvu, Salum Kinje pamoja na Nassor Saidi, Chollo.

= Dakika ya kwanza mchezo umeanza Wangono wameanza kipute
tusubiri kitachoendelea.

STARS KUIVAA BOTSWANA

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Agosti 15 mwaka huu itapambana na Botswana (Zebras) katika mchezo maalumu wa Kalenda ya FIFA utakaofanyika jijini Gaborone.
 
Tayari Kocha Kim Poulsen alishatangaza kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Agosti 8 mwaka huu tayari kwa mechi hiyo ya kirafiki ya kujipima nguvu.

FIFA KUTOA DOZI YA UTAWALA TENA.

Kozi ya Uongozi na Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itafanyika Msimbazi Center jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 6-11 mwaka huu ikiwa na washiriki 30.
 
Washiriki wa kozi hiyo itakayonedeshwa na wakufunzi kutoka FIFA ni viongozi kutoka TFF, Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, klabu za Ligi Kuu na viongozi wa mpira wa miguu wa wanawake.
 
Walioteuliwa kushiriki ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, Rais wa ZFA Amani Makungu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Ahmed Mgoyi, Blassy Kiondo, Stanley Lugenge, Khalid Abdallah, Hussein Mwamba na Eliud Mvella.
 
Wengine ni Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Salum, Katibu Msaidizi wa ZFA, Masoud Attai, wenyeviti wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal Malinzi), Dodoma (Nassoro Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).
 
Makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Mara (Mugisha Galibona), Mtwara (Vincent Majiri), Morogoro (Hamisi Semka), Kagera (Salum Chama), Tanga (Beatrice Mgaya) na Dodoma (Stuart Masima). Pia yumo Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Hilal na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.
Washiriki wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni, Ofisa Habari, Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na Matukio, Jimmy Kabwe, Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba, Ofisa Sheria wa TFF, Neema Lucumay, Ofisa wa Mpira wa Miguu wa Wanawake, Grace Buretha, Amina Karuma (Mpira wa miguu wa wanawake) na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.
 

MILION 40 KUTUMIKA MICHUANO YA ABC

Bingwa wa michuano ya BancABC Super 8 inayoanza keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) katika miji ya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza na Arusha atapata sh. milioni 40 wakati makamu bingwa sh. milioni 20. Pia timu mbili zitakazoishia hatua ya nusu fainali kila moja itapata sh. milioni 15 wakati zilizobaki kila moja itapata sh. milioni 5.
 
Timu zimepangwa katika makundi mawili ya A na B. Kundi A lina timu za Simba (mabingwa wa Tanzania Bara), Jamhuri, Zimamoto na Mtende zote za Zanzibar. Kundi ni Super Falcon (mabingwa wa Zanzibar), Azam, Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zote za Tanzania Bara.
 
Mechi za ufunguzi keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) ni Simba vs Jamhuri (Dar es Salaam), Zimamoto vs Mtende (Mwanza), Mtibwa Sugar vs Polisi Morogoro (Arusha) na Super Falcon vs Azam (Zanzibar). Awali mashindano yalikuwa yaanze Agosti 4 mwaka huu lakini yamesogezwa mbele kwa siku moja.
 
Hatua ya makundi itamalizika Agosti 12 mwaka huu. Mechi za nusu fainali na fainali zote zitachezwa Dar es Salaam. Nimeambatanisha ratiba.
 
Mdhamini bancABC atagharamia usafiri wa ndege kwa timu zote kutoka kituo kimoja hadi kingine, malazi na jezi. Yanga imejitokea kwenye mashindano hayo na nafasi yake imechukuliwa na Mtibwa Sugar ambayo ilishika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.

24 KUSHIRIKI LIGI DARAJA LA KWANZA

Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuanzia msimu huu wa 2012/2013 itakuwa na timu 24 kutokana na mabadiliko ya mfumo wa mashindano yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
 
Kamati ya Utendaji ya TFF ilikutana Julai 29 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine ilifanya mabadiliko ya mfumo wa mashindano ikiwemo FDL kuchezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini badala ya ule wa awali wa vituo.
 
Kutokana na mabadiliko hayo, timu za FDL zitagawanywa katika makundi mawili ya timu 12 kila moja kutokana na ukaribu wa kanda na kucheza kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
 
Timu ya kwanza kutoka kila kundi itapanda kucheza Ligi Kuu msimu unaofuata wakati ya tatu itakayoungana na hizo mbili itapatikana kwa mechi za nyumbani na ugenini kwa timu zilizoshika nafasi ya pili katika kila kundi.
 
Ili kufikisha idadi ya timu 24 kwenye FDL, Kamati ya Utendaji ya TFF kwa kuzingatia mapendekezo ya Kamati ya Mashindano imeamua timu tatu za juu kwenye Ligi ya Taifa kutoka vituo vyote vitatu vya ligi hiyo zimepanda daraja.
 
Sasa timu 24 za FDL ni Ashanti United (Dar es Salaam), Burkina Moro (Morogoro), Green Warriors (Dar es Salaam), Kanembwa JKT (Kigoma), Kurugenzi Mafinga (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mbeya City (Mbeya), Mkamba Rangers (Morogoro), Mlale JKT (Ruvuma) na Morani (Manyara).
 
Nyingine ni Moro United (Dar es Salaam), Mwadui (Shinyanga), Ndanda (Mtwara), Pamba (Mwanza), Polisi (Arusha), Polisi (Dodoma), Polisi (Iringa), Polisi (Mara), Polisi (Tabora), Rhino Rangers (Tabora), Small Kids (Rukwa), Tessema (Dar es Salaam), Transit Camp (Dar es Salaam), Villa Squad (Dar es Salaam)
 
Timu nne zitashuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa. Timu hizo ni mbili zilizoshika nafasi za mwisho kwa kila kundi. Timu nne zitakazopanda kucheza FDL zitapatikana kwa mchujo utakaohusisha mabingwa wa mikoa.
 
Kwa mfumo huo mpya wa mashindano, ligi za mikoa zitakazosimamiwa na kuendeshwa na vyama vya mpira wa miguu vya mikoa zinatakiwa kuwa na timu zisizopungua 16 na zisizozidi 20. Ligi za mikoa pia zitachezwa mwaka mzima kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini).
 
Ligi ya mkoa itashusha timu mbili na kupandisha nyingine mbili kutoka ligi ya wilaya. Ligi za wilaya zitakazosimamiwa na kuendeshwa na vyama vya mpira wa miguu vya wilaya zinatakiwa kuwa na timu zisizopungua 10 na zisizozidi 20.
 
Kwa wilaya zenye timu zaidi ya 20, chama husika cha mpira wa miguu kitapanga utaratibu wa kuzichuja kwa mashindano ili kupata zile bora 20 zitakazocheza ligi rasmi ya wilaya.
 
Mabingwa wa wilaya katika mkoa husika watacheza mechi za kuchujana (play offs) ili kupata timu mbili zitakazopanda daraja kucheza ligi ya mkoa husika.
 
Kutokana na mabadiliko hayo ya mfumo wa mashindano, sasa madaraja rasmi ya ligi ni Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Mkoa (Ligi Daraja la Tatu) na Ligi ya Wilaya (Ligi Daraja la Nne).
 
TFF inasisitiza kuwa kwa mujibu wa kalenda yake ya matukio, kipindi cha usajili wa wachezaji kwa madaraja yote ni kimoja, na ligi zitachezwa kwa wakati mmoja.
 
Usajili wa hatua ya kwanza ni kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu wakati kipindi cha pili cha usajili ni Agosti 21 hadi Septemba 4 mwaka huu. Usajili wa dirisha dogo ni Novemba 15 hadi Desemba 15 mwaka huu.
 
Ligi kwa madaraja yote zitaanza Septemba. Ligi Kuu itaanza Septemba Mosi mwaka huu, Ligi Daraja la Kwanza ni Septemba 15 mwaka huu, Ligi ya Mkoa na ile ya Wilaya zenyewe zitaanza Septemba 8 mwaka huu.
 
Mechi za kufungua msimu kwa madaraja yote (Ngao ya Jamii) ambazo kwa sasa zinakutanisha bingwa na makamu bingwa zitachezwa Agosti 25 mwaka huu wakati michuano ya Kombe la FA itaanzia wilayani Septemba 24 mwaka huu.

NGASA ATAMBUISHWA MSIMBAZI



Kwa upande mwingine mshambuiaji mpya wa Simba Mrisho Ngassa, leo amekabidhiwa jezi namba 16 atakayokuwa akiitumia kwenye klabu yake msimu huu.

Ngassa alikabidhiwa jezi yake hiyo katika makao makuu ya Simba Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu.

Kaburu aliongeza kwa  kusema kuwa Simba inamkaribisha Ngassa kwa moyo mmoja na kwamba wapenzi wote wa Wekundu wa Msimbazi wana imani kubwa naye kwani uwezo wake mkubwa wa soka unafahamika ndani na nje ya nchi.

Tunashukuru kwamba tumekidhi vigezo vyote vilivyohitajika kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyu. Tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumaliza muda wa mkopo wake kutoka Azam na ni imani yetu kwamba ujio wa Ngasa utaimarisha zaidi timu kwani yeye ni miongoni mwa wachezaji ambao Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, anawapenda," alisema. 

Akizungumza katika tukio hilo, Ngassa alisema amefurahi kusajiliwa na Simba kwani ni sawa na historia kujirudia, akikumbusha kwamba baba yake mzazi, Khlfan Ngassa, aliwahi kuwa mchezaji wa klabu katika miaka ya 1990.

Kabla ya mkutano huo na waandishi wa habari, Ngassa alifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Simba katika ufukwe wa Coco, jijini Dar es Salaam ambako Simba inaendelea na mazoezi yake chini ya makocha Amatre Richard na James Kisaka.

SIMBA YANADI USALAMA KWENYE MKUTANO MKUU


Klabu ya samba imetangaza rasmi kufanya mkutano mkuu wa wanachama Wote wa Simba utakaofanyika Agosti tano mwaka huu katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay kama ilivyopangwa.

Mipango yote kwa ajili ya mkutano huo muhimu kikatiba imekamilika na klabu inawaomba wanachama wake wote hai kuhudhuria mkutano huo muhimu.

Uongozi umepanga kutoa mabasi kwa ajili ya kuwasafirisha wanachama wake kutoka katika maeneo mbalimbali kwenda katika ukumbi wa mikutano.

Kutakuwa na mabasi matatu kwenye eneo la Shibam Magomeni... Mabasi matatu Temeke mwisho na mabasi matatu katika makao makuu ya Simba SC Mtaa wa Msimbazi.

Pia klabu itapeleka mabasi mawili katika wilaya za Mkuranga na Kibaha kwa ajili ya kuwaleta wanachama wake walio katika mkoa wa Pwani kuhudhuria mkutano huo.

Naye mwenyekiti wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage, amewahakikishia wanachama wa Simba kwamba mkutano huo utaendeshwa kisasa na usalama umehakikishwa kwa asilimia 100 kwa vile eneo la mkutano liko chini ya Jeshi la Polisi.

Aliongeza Rage kuwa anapenda kuwahakikishia wanachama wote wa Simba kwamba mkutano huo utakuwa bora na wote watakaokuja watafurahi na kujisikia fahari kuwa washabiki wa klabu ya soka ya Simba. Kwa wale ambao wamepanga kuja kufanya vurugu kwenye mkutano huo, klabu itaviachia vyombo vya dola vifanye kazi yake," alisema.

MAUZO YA NGASA YAKAMILIKA KWA HIYARI YA NGASA MWENYEWE.

 
Kwa ufafanuzi tu biashara ya Ngasa imeisha kwa kukubali kupokea shilingi milioni 30 na gari huku akiongeza mkataba wa mwaka mmoja wa ziada mbali na mwaka mmoja wa kutumikia Simba kwa mkopo.

Wadau wengi wa soka nchini wameibuka na madai kuwa ni dili ambalo tayari limeshapangwa na klabu ya Azam kutokana na mauzo ya mkopo yalivyozingatiwa kwa pande zote tatu.
                                                      akiwa kwenye mchuma wake mpya.
Maswali yanakuja kwako je unaweza kuamini mauzo ya mkopo yaliyo lala katika pande mbili kwanza kabala ya upande wa mchezaji mwenyewe?
                                                                     kaanza kazi rasmi
Unauzngumziaje mkataba wa Ngasa na Simba ilhali hivi karibuni nyota huyo alionekana kama bado ana mapenzi na Yanga kazi kwako?

TFF YATANGAZA RAMBIRAMBI MSIBA WA MSAFIRI MKEREMI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mwamuzi wa zamani wa kimataifa Msafiri Mkeremi kilichotokea leo alfajiri (Agosti 2 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora.
 
Licha ya kuwa mwamuzi, Mkeremi aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) sasa TFF kwa vipindi viwili tofauti. Pia aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT).
 
Vilevile aliwahi kuwa mkufunzi wa waamuzi, mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) Mkoa wa Pwani.
 
Kwa upande wa vyama vya mpira wa miguu aliwahi kuwa kiongozi katika mikoa ya Tabora, Pwani na wilayani Mpanda katika Mkoa wa Rukwa.
 
Msiba wa Mkeremi uko nyumbani kwake Urambo, na kwa mujibu wa mtoto wake Masoud Mkeremi, atazikwa Jumamosi kwenye makaburi ya Msafa yaliyoko wilayani Urambo.
 
TFF inatoa pole kwa familia na kuitaka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Pia TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.
 
Marehemu aliyekuwa akisumbuliwa na presha na ugonjwa wa kisukari ameacha wajane wawili na watoto 12.  Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amina

OFFICIAL: HUU NDIO UFAFANUZI WA SAKATA LA NGASA ULIOTOLEWA NA MENEJEA WA AZAM PATRICK KAHEMELE.

Wakuu Pokeeni hiyo


Ufafanizi juu ya suala la mchezaji Mrisho Halfani Ngasa

Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa ya ufafanuzi juu ya sakata la mchezaji Mrisho Ngasa ambalo linaonekana kupotoshwa

1.     Azam FC ilitangaza kuwa biashara ya mchezaji Mrisho Ngasa ingefungwa siku ya Jumatano 1/08/2012 saa saba mchana na ilivitaka vilabu vyenye interest na mchezaji huyo kufika makao makuu ya Azam FC ofisi ndogo zilizopo kwenye kiwanda cha unga cha Azam-Mzizima zikiwa na pesa taslimu. Bei ya mauzo iliyopangwa ilikuwa ni Dola 50,000. Lakini katika mawasiliano ya email kwa makatibu wakuu wa Simba na Yanga, Azam FC iliweka bayana kuwa ilikuwa tayari kushusha bei ya mauzo na ingemuuza Ngasa kwa timu ambayo dau lake lingekuwa kubwa zaidi ya mwenzake.


Kwa maana hiyo biashara ya mchezaji mrisho ngasa ilifanyika kwa uwazi. Lengo la Azam FC lilikuwa ni kutoa haki kwa kila klabu yenye uwezo wa kifedha kuweza kupata huduma ya Ngasa.


Pia tunaomba ifahamike bayana kuwa mchezaji Mrisho Ngasa alipewa taarifa kuwa anauzwa na aliombwa asaidie kushawishi klabu anayoitaka ifike kwetu na ofa yake. Ngasa alitamka bayana kuwa yupo tayari kwenda klabu yoyote ambayo Azam FC itaona imekidhi mahitaji yake kwa masharti kuwa maslahi yake ya kimkataba kati yake na Azam FC yazingatiwe.

2.     Hadi kufikia siku ya Jumatano 01/08/2012 saa saba mchana. Ni klabu ya Simba pekee iliyojibu kwa maandishi na kuonesha nia ya kumchukua Ngasa. Yanga wao hawakuwahi kujibu email, ingawa kwa majibu ya simu Mjumbe wao wa Kamati ya usajili Bw Sefu Magari alitangaza kuwa Ngasa hana thamani ya zaidi ya milioni 20. Na Yanga haikuwa tayari kuboresha ofa yake.

3.     Muda wa kufungwa kwa biashara ya kumuuza Ngasa ulipofika, ni simba pekee kupitia kwa makamu Mwenyekiti wake Bw Geofrey Ngange na Mhasibu wake ndiyo waliofika wakiwa na pesa taslimu shilingi milioni 25. Yanga hawakuonekana na hawakutaka kupokea hata simu walizokuwa wakipigiwa kuulizwa kama wana interest.


4.     Kikao cha dharura cha Azam FC kilikaa na kuamua kuwa biashara ya kumuuza Ngasa ilishindikana kutokana na kutokupatikana kwa mnunuzi mwenye dola 50,000. Kwa maana hiyo Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo kwenye klabu iliyofika na kuonesha nia ya kumhitaji (Simba)
5.     Simba walipewa sharti la kuhakikisha wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh 2,000,000) pamoja na stahiki zake nyingine zote za kimkataba

6.     Sababu za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam FC ingetoa kwa Ngasa kama angebaki.


7.     Azam FC inapenda kuweka wazi kuwa haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba kama inavyopotoshwa. Kama Ngasa anataka kuvunja mkataba wake au kama Yanga bado wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FC itawauzia kwani licha ya kwamba amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni mali ya Azam FC

8.     Tunaomba kuweka msimamo wetu kuwa hatupo tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba wake na hatuna sababu ya kufanya hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda tunakompeleka Azam FC inamruhusu kubakia klabuni na kutumikia adhabu.


9.     Lakini Ngasa na washauri wake waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC haipotayari kumvisha jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu wa nidhamu.

10. Kwa Sakata hili limeanza kuhusishwa na sakata la Mchezaji ramadhani Chombo. Naomba nitoe ufafanuzi kama ifuatavyo. Redondo alipewa option tatu za kuchagua baada ya kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu timu ilipokuwa safarini Mwanza.
a.     Kupelekwa kwa mkopo Moro United?
b.     Kupatikana kwa mnunuzi mwenye shilingi milioni 40
c.      Kukubali adhabu ya kufungiwa kwa miezi mitatu na kulipwa nusu mshahara wahati akitumikia adhabu.
Redondo alithibitisha kuipenda Azam FC kwa kukataa kuuzwa au kupelekwa kwa mkopo. Alikubali kutumikia adhabu yake na ilipoisha alirudi na kuomba msamaha na sasa ni mmoja kati ya wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu sana. Azam FC inajivunia kuwa na mchezaji kama Redondo na bila kupepesa macho wala kung’ata maneno. Azam FC inamchukulia Redondo kama mtu spesho na mwenye mapenzi ya dhati na klabu yake na inamtaka aendelee kuwa na moyo huo.

Imetolewa na utawala.
Azam FC


NGASA KUGOMA KWENDA SIMBA.


Usajili wa Mrisho Ngasa ndani ya klabu ya Simba bado ni kitendawili hii ni baada ya nyota huyo kuonekana kutokubaliana na maamuzi ya Azam FC kumuuza mchezaji huyo bila ya makubaliano nay eye binafsi .

Habari iliyojificha inasema kuwa nyota huyo alikutwa akitamka kuwa hata yeye mwenyewe ana ubavu wa kujiununu na yupo radhi kuvunja mkataba au kubaki Azam hadi mkataba wake umalizike na ajiunge na klabu anayoipenda.

Kwa upande wa uongozi wa Yanga, kupitia msemaji wake Luis Sendeu wanaimani kuwa wata mnyakua mshambuliaji huyo bila ya malipo yoyote kwa kuwa na imani Ngasa bado ni mali yao katika medani ya soka la Tanzania.

Ngasa aliuzwa kwa mkopo mchana wa jana kwa dau la shilingi milioni 25 kwa makubaliano ya pande mbili kati ya uongozi wa Simba na Azam fc. Huku taratibu zikidaiwa kukiukwa kwa kuwa Ngasa hakushirikishwa katika hilo.

Tukio hili linakwenda sambamba na lile la nyota wa zamani wa Simba, Mohammed Banka, Meshack Abel walipotaka malipo yao baada ya Simba kutaka kuwauza kwa mkopo. Lakini Julias Mrope wa Yanga alipokataa kuzwa Moro kwa mkopo.

HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUA, NGASA KATUA RASMI SIMBA.


Mshambuliaji nguli wa timu ya Azam na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ametangazwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa klabu ya Simba kwa mkopo baada ya klabu ya Azam kukubali kupokea ofa ya shilingi milioni 25 toka kwa wekundu hao.

Ofa hiyo iliyotangazwa kwa takribani siku nne tangu mchezo wa fainali umalizike ambapo mauzo hayo yalizingatia tamaa ya kuitaka kuichezea klabu yake ya zamani ya Yanga.

Kwamujibu wa taarifa zilizopo chini ya Kapeti zinasema kuwa mshambuliaji huyo amegoma kwenda Simba na sasa yupo kwenye mipango ya kurudi kwao mwanza kupumzika.

Kiasi  cha dola elfu hasmini za kimarekani zilitangazwa kama dau la mauzo ya moja kwa moja kwa nyota huyo mahiri wa Azam.

SIMBA YAKARIBIA KUMNUNUA NGASA, HUKU KOCHA AKIFUANGIWA VIRAGO VYAKE.


Uongozi wa klabu ya Azam umekana taarifa za kumuuza mchezaji abubakary Salum Sure Boy .
Hayo yamesemwa na kutihibisha mchana wa leo na msemaji wa Azam Japha Iddi Maganga baada ya kusambaa kwa taarifa za kufukuzwa kwa kocha wa timu hiyo raia wa England.

Maganga amesema suala la kufuukuzwa kocha ni kweli kocha ametisitishiwa mkataba wake na nafasi yake imeshikwa na kocha msaidizi Kally Ongala huku upande wa Sure Boy klabu hiyo haijatangaza chochote juu ya mauzo ya nyota huyo.

Kwa upande wa mshambuliaji wake Mrisho Ngasa anayesadikiwa kutakiwa na klabu ya jangwani huku yeye mwenye akionyesha mapenzi na timu hiyo haswa katika michuano iliyopita ya Kagame ambapo Ngasa alivalishwa jezi ya Yanga na mashabiki naye kuibusu bila ya woga, Maganga amesema nyota huyo ametangaziwa ofa yake kuwa ni  dola 50,000  za kimarekani ikiwa na maana klabu yoyote ikiwa tayari ruksa kuuziwa.

Hadi Blogu hii inaondoka kwenye maskani ya Azam klabu ya Simba ndiyo iliyokuwa ikisadikiwa kuwa inaweza ikafanya biashara na wana rambaramba wa Azam FC.

Sure boy na Ngasa walidaiwa na mashabiki kuwa walicheza chini ya kiwango kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Yanga huku kocha akidaiwa na wadau hao kwamba alifanya kinyume kumchezesha Ngasa kwenye mchezo wa fainali.

CHUJI ARUDI STARS KWA KISHINDO.


Hii leo kocha mkuu wa wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya mechi ya kirafiki itakayochezwa ugenini Agosti 15 mwaka huu.
 
Wachezaji walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambi kwenye hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam, Agosti 8 mwaka huu saa 1 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza siku inayofuata.
 
Makipa walioitwa kwenye kikosi hicho ni Deogratias Munishi (Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha msaidizi Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
 
Viungo ni Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi (Simba), Mrisho Ngassa (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
 
Wachezaji wanaounda safu ya ushambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Said Bahanuzi (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).

Katika kikosi hiki klabu ya Azam bado kinara kwa kutoa wachezaji wengi ambapo imetoa takribani wachezaji nane.

Katika kimetawaliwa na badiliko kubwa moja la  kuitwa kwa Athumani Iddi Chuji alieachwa kwenye timu tangu enzi za Maximo kocha wa zamani wa timu hiyo.