
Kocha wa zamani wa Yanga Roul Shungu akisifu kikosi cha Yanga. Kwa jinsi inavyojituma na kuwa na utulivu wa katika suala la umaliziaji ikiwa mchezoni. Shungu amesema hayo mwishoni mwa juma lililopita mara baada ya yanga kutwaa ubingwa wa soka wa Kagame dhidi ya Azam FC ambapo Yanga ilishinda magoli 2 kwa 0.
Shungu amesema wachezaji waliosajiliwa na Yanga wanaakili za kiushindani na nidhamu ya mashindano ndio maana wanajituma sana huku akitoa mfano jinsi washambulijia wa Yanga Saidi Bahanuzi na Hamisi Kiiza wanavyopamba hadi kuhakikisha wanashinda michezo hiyo.
Mbali na hayo Shungu amesema kuwa yeye tupo tayari kurejea nchini kwa kazi hiyo kwa kuwayeye ni sehemu ya Tanzania kutokana ameoa hapa nchini na familia yake inaishi hapa nchini.
Lakini pia amefungua milango ya usajili kwa vilabu vinavyo hitaji wachezaji wao huku akiwa na imani kwamba wao wana nyota wengi katika timu yake ya AS Vita ambayo anaifanyika kazi kama mkurugenzi wa ufundi.
0 comments:
Post a Comment