
Siku chache baada ya TFF kungaza kuwepo kwa michezo miwili ya kirafiki kwa timu ya taifa ya vijana Ngorongoro Heroes huku ratiba ikionyesha itacheza mechi na Misri michezo hiyo imefutwa.
Chama cha Mpira wa Miguu Misri (EFA) kimetuma taarifa hiyo jana kikiomba kusogezwa mbele hadi mwishoni mwa Agosti baada ya kushindwa kupata usafiri wa ndege kuwahi tarehe ambazo ilikubaliana na TFF kwa ajili ya mechi hizo.
Ngorongoro Heroes ambayo tayari iko kambini ilikuwa icheze mechi hizo Julai 3 na 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kuikabili Nigeria katika mechi ya michuano ya Afrika, Julai 29 mwaka huu.
Mechi nyingine za kirafiki kwa Ngorongoro Heroes inayofundishwa na Jakob Michelsen zitachezwa Julai 14 na 16 mwaka huu dhidi ya Rwanda.
Kufutwa kwa michezo hiyo nifursa tosha kwa Ngorongoro kutafuta michezo mingine na siku kukaa chini
0 comments:
Post a Comment