KAVUMBAGU NDANI YA YANGA.


Yanga ya msajili Kavumbagu kwa mkataba wa miaka miwili.
Kutoka katika chanzo cha kuaminika cha habari Didier Kavumbagu amesaini mkataba huo siku ya julai 28 ikiwa ni saa chache tu kabla ya mechi ya fainali kuanza kati ya Yanga na Azam FC.

Kavumbagu anatarajiwa kujiunga na kikosi cha Yanga rasmi siku ya Jumatatu ya wiki ijayo.

YANGA YAKEMEA VURUGU ZA MASHABIKI.


Baada ya kutwaa ubingwa ligi ya mabingwa afrika ya mashariki, Kagame Cup uongozi wa mabingwa wa kombe la kagame Dar es Salaam Young Afrika umekemea kitendo cha mashabiki wa Yanga kufanya fujo katika mchezo wa fainali kati yao dhidi ya Azam FC mchezo uliopigwa juma lililopita.

Msemaji wa Yanga Luis Sendeu amesema uchunguzi juu ya jambo hilo unaendelea na ikibainika kuwa walianza mashabiki wa yanga hatua kali zitachukuliwa.

Kwa upande mwengine Sendeu amefunguka juu ya timu hiyo na kusema kwa wachezaji wa Yanga wamepewa likizo ya wiki moja inayotarajiwa kumalizika siku ya ijumaa.

SHUNGU AMESEMA HAYA KUHUSU YANGA NA TIMU ZA BONGO.


                            
Kocha wa zamani wa Yanga Roul Shungu akisifu kikosi cha Yanga. Kwa jinsi inavyojituma na kuwa na utulivu wa katika suala la umaliziaji ikiwa mchezoni. Shungu amesema hayo mwishoni mwa juma lililopita mara baada ya yanga  kutwaa ubingwa wa soka wa Kagame dhidi ya  Azam FC ambapo Yanga ilishinda magoli 2 kwa 0.

Shungu amesema wachezaji waliosajiliwa na Yanga wanaakili za kiushindani na nidhamu ya mashindano ndio maana wanajituma sana huku akitoa mfano jinsi washambulijia wa Yanga Saidi Bahanuzi na Hamisi Kiiza wanavyopamba hadi kuhakikisha wanashinda michezo hiyo.

Mbali na hayo Shungu amesema kuwa yeye tupo tayari kurejea nchini kwa kazi hiyo kwa kuwayeye ni sehemu ya Tanzania kutokana ameoa hapa nchini na familia yake inaishi hapa nchini.
Lakini pia amefungua milango ya usajili kwa vilabu vinavyo hitaji wachezaji wao huku akiwa na imani kwamba wao wana nyota wengi katika timu yake ya AS Vita ambayo anaifanyika kazi kama mkurugenzi wa ufundi.

NGORO YAAHIDI USHINDI MECHI YA LEO


 
Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) imeahidi ushindi kwenye mechi yake dhidi ya Nigeria (Flying Eagles) itakayochezwa leo jioni kwenye uwanja wa taifa.
 
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo zitakazofanyika mwakani nchini Algeria itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
 
kwa upande wake kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Jakob Michelsen na nahodha wake Omega Seme wamesema timu yao iko tayari kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Kenya.
 
Michelsen amesema timu yake imepata mechi mbili za kujipima nguvu dhidi ya Rwanda, lakini pia aliishuhudia Flying Eagles ikicheza mechi ya kirafiki na Rwanda (Young Amavubi) uliofanyika Julai 24 mwaka huu jijini Kigali.
 
“Timu iko vizuri na wachezaji kama Frank Domayo, Simon Msuva na Ramadhan Singano ambao pia wanachezea timu A (Taifa Stars), hivyo uzoefu wao ni muhimu kwa mechi ya kesho.
 
Nigeria ni mabingwa watetezi wa michuano hii kwa hiyo tunatarajia upinzani mkubwa, lakini tumejiandaa kwa hilo. Nigeria ni nchi yenye mfumo mzuri wa timu za vijana, na sisi tunaelekea huko huko” amesema Michelsen.
 
Naye Kocha Mkuu wa Flying Eagles, John Obuh amesema haijui vizuri Ngorongoro Heroes lakini anaiheshimu kutokana na ukweli kuwa inacheza raundi ya pili baada ya kuitoa Sudan katika raundi ya kwanza.
 
“Sina mchezaji yeyote anayecheza mpira wa kulipwa nje ya Nigeria, lakini tumekuja kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kucheza raundi ya mwisho na hatimaye tucheze fainali mwakani,” amesema Obuh aliyefuatana na nahodha wake Samuel Okan ambaye ni mlinda mlango.
 
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Moses Osano ni sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C itakuwa sh. 5,000. Kiingilio kwa VIP A ni sh. 10,000.
 
Osano atasaidiwa na Peter Keireini na Elias Wamalwa wakati mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Thomas Onyango. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Charles Masembe kutoka Uganda.
 
CAF YAMTEUA HAFIDH ALI KUSIMAMIA MECHI YA WASUDAN
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua mwamuzi wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Hafidh Ali kuwa Kamishna wa mechi kati ya El Ahly Shandy na Al Hilal zote za Sudan.
 
Shandy ndiyo mwenyeji wa mechi hiyo namba 98 ya Kombe la Shirikisho itafanyika Agosti 5 mwaka huu na itachezwa Uwanja wa Shandy ulioko katika mji wa Shandy.
 
Mwamuzi wa mechi hiyo ni Raj Seechun kutoka Mauritius ambaye atasaidiwa na Balkrishna Bootun, Jean Daniel Telvar na Parmendra Nunkoo, wote pia kutoka Mauritius. Mratibu Mkuu wa mechi hiyo ni Paul Bassey wa Nigeria.
 

YANGA BINGWA TENA WA KAGAME 2012.



Haya ni makubwa mno yaliyotokea kwenye uwanja wa taifa baada ya vichapo vitatu kuikumba Yanga toka kwa Azam FC hii leo wana jangwani ikiwa ni siku kumi na tatu tangu kupata uongozi mpya Yanga yavunja uteja kwa Azam baada ya kufinga magoli 2 kwa 0 na kutwaa taji la Kagame Cup 2012.

Kwa ushindi huo Yanga imechora ramani ya mpya ya kutwaa taji hilo ma mbili mfululizo ikichagizwa na msimu uliopita ambapo Yanga ilitwaa ubingwa huo mbele ya Simba baada ya kushinda goli moja lilifungwa na Keneth Asamoh kwa kuitumia pasi safi ya rashidi Gumbo.

Kabla ya kuanza kwa pambano hilo yanga tayari ili ahidiwa kiasi cha million 30 kama posho ya kuichapa Azam FC.

YAMETIMIA MANJI ASHINDA RASMI RUFAA.


                                  
Baada ya kikao cha kamati ya jana na leo jumatatu ili kupitia rufaa aliyokatiwa mgombea nafasi ya uenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji na Ishabakaki Lutta kamati ya hiyo hii leo imetoa jibu juu ya rufaa hiyo.

Katia majibu hayo ya kamati huku ikipitia ibara ya 11 kipengele cha pili imesema kuwa mrufani akutoa vielelezo vya kutosha na kuweka anuani ya kudumu ya rufaa yake.

Nakutokana mrufani hakutokea kutetea rufaa hiyo kamati imeamua kutupilia rufaa hiyo na kuleta maana kuwa Manji atagombea nafasi yake.

FUNUNU NZITO YA KIBONGO.


 
Tetesi yenye kuaminika inaeleza kuwa mgombea uenyekiti wa Yanga Yusuph Manji ashinda rufaa yake hii ni baada ya kikao cha leo.

HAYA NI YA COPA COCA COLA.


Timu ya Ruvuma imethibitisha kuwa mwiba mkali katika michuano ya Copa Coca-Cola mwaka huu baada ya leo asubuhi (Julai 2 mwaka huu) kuishushia Lindi kipigo cha mabao 7-2.
 
Hadi mapumziko kwenye mechi hiyo ya kundi A iliyochezwa Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani, washindi ambao kwa matokeo hayo wamejiweka katika nafasi nzuri ya kucheza 16 bora walikuwa mbele kwa mabao 3-0.
 
Waliotikisa nyavu ni Anthony Christian dakika ya 23 na 50, Edward Songo dakika ya 27, 75 na 86 na Sunday Leonard dakika ya 32 na 60. Mabao ya Lindi yalifungwa na Salum Mnyamwile dakika ya 18 kwa njia ya penalti na lingine dakika ya 48 kupitia kwa Mwarami Maundu.
 
Nayo Tanga imepata ushindi wake wa kwanza katika michuano hiyo baada ya kuifunga Manyara mabao 2-0 katika mechi ya kundi B iliyochezwa Uwanja wa Tamco mkoani Pwani. Mabao ya washindi yalifungwa na Mbwana Musa dakika ya 47 na Issa Mwanga dakika ya 60.
 

INIESTA MCHEZAJI BORA ULAYA.


 Andres Iniesta
Mara baada ya mashindano kiungo wa Hispania Andres Iniesta ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo makubwa barani ulaya.
Uteuzi huo umezingatia maadili ya mchezo wa soka kutoka kwa kamati ya ufundi ya michuano hiyo.