
Yondani akiwa na jezi ya Yanga.
Taarifa yenye
kusikitisha kwa mashabiki wa klabu ya soka ya Yanga kuwa mlinzi wa klabu hiyo
Calvin Yondani amepasuka mfupa wa mguu wake wa kulia baada ya kugongwa na
kiungo wa Simba Haruna Moshi Boban katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa juzi
kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na
Blog hii daktari wa timu ya Yanga Juma Sufiani amesema kuwa jeraha hilo
litamgharimu takribani wiki zisizo pungua mbili kukaa nje ya uwanja kwaaji ya
matibabu zaidi.
Sufiani
amesema maumivu ya mchezaji huyo ni makubwa kiasi ambacho anatembelea magongo
maalum kwaajili ya kumpa nguvu ya kusogea kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Kuumia kwa
Yondani kunatukumbusha mengi
yaliyopoteza viwango vya nyota wetu kama ilivyokuwa kwa Victor Costa wa
aliekuwa samba kipindi hicho na uhuru Selemani wa Simba, Shamte Ali wa yanga
ambaye bado wanalitumikia soka la Tanzania.
0 comments:
Post a Comment