Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Arusha (KRFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana Oktoba 7 kule
jijini Arusha.
Msemaji wa TFF Boniface Wambura amesema
kuwa viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo,kwa upande wa mwenmyekiti ni
Khalifa Mgonja, Seif Banka (Makamu Mwenyekiti), Adam Brown (Katibu), Peter Temu
(Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Omari Walii (Mwakilishi wa Klabu TFF) na Mwalizo
Nassoro (Mhazini).
Waksti nafasi ya wajumbe wa Kamati ya
Utendaji katika uchaguzi huo uliofanyika Leganga, Usa River ni Hamisi Issa,
Athuman Mhando na Eliwanga Mjema. Nafasi ya Katibu Msaidizi iko wazi na
itajazwa katika uchaguzi mdogo utakayofanyika baadaye.
Amesema TFF inaahidi kuendeleza
ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya ARFA chini ya Mwenyekiti wa Khalifa
Mgonja ambaye amechaguliwa tena kuongoza chama hicho.
0 comments:
Post a Comment