Mwanadada wa Uingereza, Laura Robson
amefanikiwa kufuzu raundi ya pili ya michuano ya Japan Open baada ya kumfunga Mgiriki, Eleni Daniilido
kwa seti 6-4,6-2.
Laura mwenye umri wa miaka 18 akiwa katika nafasi ya 56
duniani atakutana na mwanadada wa kichina, Zhou Yimiao katika mchezo wa raundi
inayofuta.
Robson huenda akashika nafasi ya 50 kwa ubora kama atwaa
mataji yanayokuja ukijumuisha na ushindi wa medali alizoshinda kwenye michuano
Olimpic.
Kumbuka kuwa Robson aliikosa kushika nafasi ya 50, baada ya
kufungwa na Su Wei wa china katika fainali Guangzhou Open na kushindwa kuvunja
rekodi ya muingereza Sara Gomer alietwaa
taji hilo kwa mara ya mwisho mwaka 1988.
0 comments:
Post a Comment