JESHI LA SERBIA LA KINUKISHA KWA WACHEZAJI WA ENGLAND



Jeshi la polisi la nchini Serbia limewatia hatiani watu 12 wakiwemo wachezaji wawili wa timu ya taifa ya England chini ya umri wa miaka 21 kwa tuhuma kusababisha vurugu kwenye mchezo kati ya England na Serbia wakufuzu fainali za ulaya mwaka 2013.
Jeshi hilo halikuweka bayana majina ya watu hao ila imeeleza kuwa katika orodha hiyo wamo wachezaji watano wa timu ya Serbia, makocha wa wasaidizi wa timu zote mbili sambamba na wachezaji wawili wa England.
Kwa upande mwingine jeshi limesisistiza kuwa walioingizwa katika kesi hiyo ya jinai ndio walio thibitishwa na kuanzisha vurugu kutokana na uchunguzi uliofanywa na polisi wa jiji la Krusevac kwa muda wa wiki mbili
Kwa upande wa chama cha soka cha nchini England FA, kimesema kuwa mpaka sasa hawajapokea maelezo yoyote juu ya kesi hiyo na kwasasa wanasubiri maelezo kamili ili waweze kutoa tamko.
Katika mchezo huo wa kuwania tiketi ya michuano ya ulaya ya mwaka 2013 uliochezwa jijini Krusevac nchini Serbia, Octoba 16 mwaka England iliifunga Serbia magoli 1kwa 0

0 comments:

Post a Comment