Mashambuliaji wa Real Madrid Cristian Ronaldo, ameruhusiwa
kuitumikia timu yake ya taifa ya ureno, katika mchezo wa kimataifa kuwania
kufuzu fainali za kombe la dunia mwaka 2014 kule nchini Brazil.
Ronaldo amepewa ruhusa hiyo na jopo la madaktari wa klabu yake
ya Real Madrid baada ya kugundulika kuwa amepona jeraha la bega alilolipata
katika mchezo wa jumapili dhidi ya Barcelona.
Baada ya sare ya magoli kwa 2 kwa 2 ya El Classico, kocha wa
timu ya taifa ya Ureno Paul Bento alikata tama ya kumtumia mchezaji huyo baada
ya kusikia ameumia bega mbalina kumaliza dakika zote 90.
Oktoba 12 kikosi cha Ureno kitakuwa ugenini mjini Moscow kucheza
na timu ya taifa Urusi katika mchezo huo wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za
kombe la dunia 2014.
0 comments:
Post a Comment