TFF YAITUPA RUFAA MGONGOLWA.

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, imetupilia mbali rufani iliyowasilishwa na warufani Mussa Mahundi, Abou Silia na Alex Mgongolwa, dhidi ya kamati ya uchaguzi ya chama cha mpira mkoani Iringa IRFA.

Warufani hao waliokuwa wakiwania nafasi za uongozi wa soka mkoani Iringa waliitaka kamati ya TFF, kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa IRFA, uliofanyika September 8 mjini Mufindi, sambamba na kuomba uchaguzi ufanyike upya chini ya kamati ya uchaguzi ya TFF.

Baada ya kupitia rufaa hiyo, mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF, Deogratius Lyato ameeleza kuwa rufaa hiyo imekosa sifa ya kamati yake kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za TFF ibara ya kwanza 8 (2) ibara 21(3) na ibara ya 24(2) kwa kutozingatia matakwa ya kanuni za chaguzi za wanachama wa TFF.

Lakini pia Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya IRFA kuchukua hatua dhidi ya mdau wa michezo, Abuu Changawa kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, Ibara ya 28(6) kwa kuingilia mchakato wa uchaguzi wa IRFA siku ya uchaguzi.

0 comments:

Post a Comment