Petrova akiwa kazini
Michuano
ya Pacific hii leo imefifikia tamati kwa mchezo wa fainali uliowakutanisha
mwanadada Nadia Petrova wa Urusi na Agnieska Radwanska wa Poland.
Katika
mchezo huo Nadia Petrova amefanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kumfunga mtetezi wa taji hilo Agnieska Rwandaska kwa
seti 6-0,1-6, na 6-3 na kumuwezesha kutwaa taji la 12 katika maisha yake ya
Tennis.
Nadia
mwenye umri wa miaka 30 akiwa ameshika nafasi ya 17 aliingia fainali baada ya
kumfunga Sam Stosur Astralia kwa seti 6-4,6-3 huku mpinzani wake,Agnieska Rwandaska
akiingia hatua hiyo kwa kumfunga Angelik Kerber kwa seti 6-1,6-1,
Baada
ya mchezo Nadia amesema ilikuwa ngumu sana kushinda mchezo wa leo haswa pale
alipoingia katika seti ya tatu huku wakiwa wameharibu seti moja kila mmoja
katika mechi hiyo ya mwisho.
0 comments:
Post a Comment