Kocha
wa Manchester united Sir Alex Ferguson amewakaribisha kwa pongezi kubwa nyota
wake Wayne Roony na Darren Fletcher kwa kurejea uwanjani kwa kuiletea klabu mafanikio
makubwa katika mchezo wa kwanza wa kombe la ligi.
Katika
mchezo Fagason alivutiwa na viwango vya wachezaji wake akiwemo Roony
alieonekana jana kwa mara ya kwanza tangu alipoumia mguu katika ushindi wa
magoli 3 kwa 2 dhidi ya Fulham.
Kwa
upande wa nahodha wa Scotland, Darren Fletcher ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza
aliposhindwa kuitumikia klabu hiyo tangu mwaka 2011 kutoka na kusumbuliwa na
matatizo ya tumbo.
Fagason
amesema kuwa sasa wanahitaji kuendeleza wimbi la ushindi katika mashindano yote
yanayo endelea huku akisisitiza kuwa watashinda kila mchezo muhimu wa klabu
hiyo.
Kwa
upande wa wapinzani wao wa jana Newcastle United kupitia kocha wake Alan Pardew
ameridhishwa na kurejea kwa mshambulaji wake Pappis Demba Cisse aliekuwa
akisumbulia na kifundo cha mguu.
Katika
mchezo huo wa jana Cisse alimfunga goli la kufutia machozi katika dakika
ya 62.
0 comments:
Post a Comment