Wadau wasoka mkoani Iringa wafunguka baada ya maauzi ya kamati ya uchaguzi TFF.




Siku moja baada ya kamati ya uchaguzi ya TFF kutangaza kutupilia mbali rufani ya wagombe wa nafasi za uchaguzi mkoani humo Mussa H.Mahundi, Abou O.Silia pamoja na mwanasehria Alex Mgongolwa, wadau wa soka mkoani Iringa wamewataka viongozi wa soka kushirikiana katika kulikuza soka la mkoa huo.
Akizungumza na Mwananchi mdau wa mchezo huo Juma Mpiluka amesema  kwa sasa kilichobaki ni kuacha malumbano na kushirikiana na uongozi wa IRFA ilikujenga sura bora ya soka la Iringa lililo poteza dila ya kitaifa tangu mwaka 1999 timu ya Lipuli ya Iringa Iliposhuka daraja.
Mdau huyo aliongeza kuwa ni vema uongozi  huo mpya chini ya mwenyekiti wake Cyprian Kuyawa kuitisha mkutano wa wadau wa michezo ili kukusanya mawazo chanya yatakayoweza kuleta mabadiliko katika soka la Iringa. Sambamba na kuutaka uongozi uwateue wagombea walioshindwa katika kamatii mbalimbali za uongozi ili kupata fursa ya kutumia mawazo na sera zao zilizo shindwa kufua dafu kwenye uchaguzi.
Kwa upande wa mdau mwingine alikataa kutajwa jina lake alisema kuwa suala la kushindwa kwa rufani hilo lilikuwa lipo wazi kutokana nguvu ya katibu wa chama soka mkoani Iringa Eliudi Mvela ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji TFF taifa kuwa tayari cheo chake kinaweza kutoa maamuzi huku kanuni ikipindishwa, sema kilichobaki ni kuongeza mshikamano wa nguvu kwa wadau wote wa Iringa na kuboresha mchezo huo.
Kwa sasa mkoa wa Iringa na IRFA una kazi kubwa ya kuhakikisha timu za Kurugenzi ya Mufndi na Polisi Iringa zinapanda ligi kuu msimu unaokuja.
Kumbuka kuwa katika uchaguzi uliofanyika September 8 kule wilayani Mufindi, wajumbe wa IRFA waliwapitisha Cyprian Kuyava katika nafasi ya uenyekiti, Stanford Mwakasala Makamu mwenyekiti, kwa upande wa katibu mkuu Eliud Mvela alierudi madarakani kwa awamu ya tatu, Abwene Mwakalobo katibu msaidizi,
Katika nafasi ya muhazini alichaguliwa Abdalah Kiyumbo, Coasta Magoroso akirudi katika nafasi ya uwakilishi wa vilabu, Ramadhani Mahano Mjumbe mkutano mkuu wakati waliochaguliwa kwenye kamati ya utendaji ni Maulidy Toffy pamoj na Festor Mwamalekela.

0 comments:

Post a Comment