Kila siku huwa najiuliza maisha ni nini na jinsi gani tunatakiwa tuishi ili tupate mafaniko bora bila kukutana na vikwazo, jibu jepesi lililotua kwenye kichwa change linasema kuwa kwa ukijitambua unaweza kupata alau jibu la maisha ni kutu gani.
Hili pia ni tatizo la vilabu vikubwa vya Tanzania nazungumzia Simba na Yanga kuwa vinashindwa kusoma alama za nyakati katika shughuli za uendeshaji wa klabu zao. Hivi leo kilele nyingi na miaka mingi huzuka kipindi kama hiki tunakumbua kelele za usajili wa Athumani Iddi Chuji, Marehemu Saidi Mwamba Kassim Issa Chim pamoja na Shibori aliotikisa vichwa msimu uliopita alafu ni galasa katika soka.
Kule barani ulaya tunaona jinsi Arsenal wanavyo haha kutafuta mbinu kumuongeza mkataba Robin Van Parse akiwa amebakisha mwaka kwenye mkataba wake huku Munich wakiongeza mktaba wa Ribery na Roben,
Manchester United wakiongeza mkata wa Dan Welbeck na Paul Scores ambao hao wote bado hawajafika kileleni mwa mikataba yao lakini Tanzania si hivyo.
Manchester United wakiongeza mkata wa Dan Welbeck na Paul Scores ambao hao wote bado hawajafika kileleni mwa mikataba yao lakini Tanzania si hivyo.
Bado haijaeleweka kama tatizo ni ubahiri ama kujiamini kupita kiasi usajili wa Yanga kwa Kelvin Yondani umezua mzozo mkubwa ambao kila kiongozi anatamba kivyake Yanga wanasema Yondani ni wao kihalali Simba nao wanadai kuwa Yondani ni mchezaji wao na amesha ongeza mkataba. Lakini ukirudi TFF unakuta kitu kinachokosoa viongozi wa soka la bongo ikiwa na maana Simba wameshinda kuongeza mkataba wa Yondani mapema kabla ya kumalizika ama kufika mwisho wa mkataba huo bado nipo kwenye bumbuazi. Au wamechukulia ile hali ya kimjini kama wachezaji walio katika timu muda mrefu wanawaweza kwahiyo hata kama mkataba ukimalizika mambo yatakuwa sawa.
Mbali na hilo ni kudokeze tu msomaji wa BLOGU HII YA TWALIB OMARY, kuwa wiki iliyopita nilizungumza na kiungo wa simba Uhuru Selemani kuhusu mkataba wake alichokijibu unagundua kama viongozi wa soka la bongo wanaridhika na kudharau baada ya mafanikio machache ya soka, Uhuru alisema kuwa yeye yupo tayari kujiunga na klabu yoyote ambayo itatoa mkataba mnono na mzigo wa maana hii inakupa picha ipi kuwa mkataba wake na Simba umemalizika na Simba hawajaanza mazungumzo yoyote na nguli huyo wa zamani wa Coast Union ya Tanga.
Naye mlinzi wa kushoto wa Simba Juma Jabu sijui ndio umemkuta ule usemi wa kipya Kinye kwa kuwa yupo Amir Maftar basi Simba bado hawajafungua mazungumzo kwa hiyo hii ni hatari kubwa inahitajika hali ya kujitambua katika usajili na unaishi na akina nani katika timu yako. Maana tumezoea kuonawachezaji wa zamani wakicheza hali ya kuwa wana damu za klabu zao mfano Abdallah Kibadeni, Ally Mayai, Mzee Abdalah na wengine wengi, lakini baadaye ikaja ile kauli ya mpira mpesa ikawaamsha wachezaji wengi na kuacha kucheza kwa mapenzi yanayorudisha nyuma mafanikio ya soka.
Lengo la kuzungumza haya si kama Simba ni wajinga haya yaliweza kujitokeza hata kwa Yanga walipo muuza Ngasa bila ya makubaliano ya benchi la ufundi halafu baadae pesa ya mauzo haikujulikana imefanya kitu gani ndani ya klabu hiyo.
Mimi Twalib naondoka maneno huenda yakawa swali kwako wewe msomaji endelea kutembelea Blogu hii kwa taarifa nyingi za kimichezo.
0 comments:
Post a Comment