Ally Mayai
Kutoka Jangwani, Beki wa zamani wa kikosi cha mabingwa wa zamani Ally Mayay Tembele aliyechukua fomu ya kuwania nafasi ya makam mwenyekiti anatarajiwa kuwekewa pinga mizi na mgombea mwenza wa nafasi hiyo.
Akizungumza na kipindi hiki mmoja wa wanachama ambaye akupenda jina lake litanjwe amesema kuwa mgombea huyo anataka kuwasilisha pingamizi kwa Kamati ya Uchaguzi, kupinga Mayay kugombea nafasi yoyote Yanga, kwa sababu uchaguzi utakaofanyika Julai 15, mwaka huu ni wa kujaza nafasi za viongozi waliojiuzulu, akiwemo Mayay mwenyewe.
Chanzo cha habari hicho kimefafanua kuwa kama ataruhusiwa kugombea atakuwa amechezea katiba kwa kuwa alijiuzulu na wajumbe wengine kama Mohamed Binda.
Waliochukua fomu katika kitimu timu hicho ni pamoja na aliyekuwa mdhamini wa Yanga Yussuf Mehboob Manji atachuana na John Jambele, Edgar Chibura na Sarah Ramadhani kwenye nafasi ya uenyekiti, wakati wapinzani wa Mayay ni Ayoub Nyenzi, Clement Sanga na aliyekuwa mbunge wa LindiYono Kevela
0 comments:
Post a Comment