WADAU WA YANGA WASHUKA JUU YA FOMU YA MANJI.

 
                     Yusuph Manji akiwa katika moja ya shuguli za Yanga
Baada ya aliyekuwa mdhamini wa Yanga kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya mwenyekiti katika mchakato wa kujaza nafasi za viongozi waliojizuru uchaguzi utakaofanyika julai 15 mwaka huu wadau na mashabiki wamefunguka kwa maoni mbalimbali.
Kassim Jumanne amesema kuwa wamuache awanie hiyo nafasi na akifanikiwa ataongoza vizuri kwasababu ana pesa.

katika maelezo yake zaidi amegusia vitu alivyowahi kufanya Manji ndani ya klabu hiyo kama Mfadhili huku akiamini kuwa anaweza akafanya makubwa katika uongozi wake.

Naye John Ndambile amesema endapo atafanikiwa wanachama wa Yanga wajue kwamba mali ni ya Manji kwa kuwa ataendesha klabu kama kampuni.

je wewe mdau unasema juu ya Manji na uongozi wa Yanga?

0 comments:

Post a Comment