Kocha wa Gambia, Luciano Mancini.
Kocha wa timu ya taifa ya Gambia Luciano Mancini amemsifu mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samata kuwa anauwezo mkubwa wa kucheza soka huku akisema kuwa kiwango cha nyota huyo si cha kucheza soka barani Afrika.
Akizungumza hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Gambia na Taifa Stars amesema uwezo wa Samata ukilinganisha na ligi anayocheza na atafanya makubwa sana akipata fursa ya kucheza na ulaya ama marekani.
Kwaupande wa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Kim Polsen amefarijika sana kwa kushinda mchezo wake wa kwanza tangu aanze kuifundisha timu ya taifa Stars.
0 comments:
Post a Comment