Mbaya wa Tomaajiriwa Yanga.




     
                             Ernie Brandts
Klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati Dar Young Africans imemtambulisha rasmi kocha wake mpya Mholanzi Ernie Brandts.

Kwa kumbukumbu ya karibu kocha huyi ndiye yule aliyekuwa kiifundisha klabu bingwa ya Rwanda APR.

 Kocha huyo amewasili jijini Dar es Salaam jana usiku na leo asubuhi ametambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari na kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha klabu hiyo ya Jangwani.

Brandts ambaye aliwahi kuwa nyota wa timu ya taifa ya Uholanzi na klabu kubwa ya nchi hiyo PSV Endoven akicheza nafasi ya ulinzi, amekuja Yanga kuchukua nafasi ya mbelgiji Tom Saintfiest aliyetimuliwa wiki iliyopita baada ya kukaa kwenye klabu hiyo kwa siku 81.

VIINGILIO VYA SIMBA NA YANGA HADHARANI.




 
Shirikisho la soka nchini TFF hii leo limetangaza viingilizo vya mechi ya Simba na Yanga.

Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumatano (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000.

Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom itachezwa kwenye uwanja huo kuanzia saa 11 kamili jioni. Watazamaji watakaotaka kuona mechi hiyo wakiwa wameketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.

Viingilio vingine kwenye mechi hiyo ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000.

Nadia atwaa Pan Pacific



                                                                 Petrova akiwa kazini
Michuano ya Pacific hii leo imefifikia tamati kwa mchezo wa fainali uliowakutanisha mwanadada Nadia Petrova wa Urusi na Agnieska Radwanska wa Poland.
Katika mchezo huo Nadia Petrova amefanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kumfunga  mtetezi wa taji hilo Agnieska Rwandaska kwa seti 6-0,1-6, na 6-3 na kumuwezesha kutwaa taji la 12 katika maisha yake ya Tennis.
Nadia mwenye umri wa miaka 30 akiwa ameshika nafasi ya 17 aliingia fainali baada ya kumfunga Sam Stosur Astralia kwa seti 6-4,6-3 huku mpinzani wake,Agnieska Rwandaska akiingia hatua hiyo kwa kumfunga Angelik Kerber kwa seti 6-1,6-1,
Baada ya mchezo Nadia amesema ilikuwa ngumu sana kushinda mchezo wa leo haswa pale alipoingia katika seti ya tatu huku wakiwa wameharibu seti moja kila mmoja katika mechi hiyo ya mwisho.

VIKOSI VYA SIMBA NA PRISON LEO




Simba:                                                  Tanzania Prisons:
01.Juma Kaseja (c)                            18.David Abdallah
02.Nassoro Masoud                             03.Aziz Sibo
17.Amir Maftah                                  05.Laurian Mpalile
15.Shomari Kapombe                          16.Lugano Mwangama (c)
24.Juma Nyoso                                   15.David Mwantika
14.Mwinyi Kazimoto                            13.Khalid Fupi
28.Amri Kiemba                                  07.Misango Magai
08.Ramadhan Chombo                         12.Fred Chudu
19.Edward Christopher                        14.Elias Maguri
10.Felix Sunzu                                     17.Peter Michael
16.Mrisho Ngasa                                   19.John Matei

Wachezaji wa akiba;
22.Wilbert Mweta                                 01.Daudi Mwasongwe
23.Paul Ngalema                                   04.Jumanne Elfadhili
20.Jonas Mkude                                     09.Sino Augustino
12.Salim Kinje                                       22.Julius Kwaga
04.Komanbil Keita                                 08.Henry Mwalugala
13.Daniel Akuffor                                   11.Hamisi Ally
05.Pascal Ochieng                                  23.Jeremiah Juma

Refa: Paul Soleji (Mwanza)
Mwamuzi Msaidizi 1: Jesse Erasmo (Morogoro)
Mwamuzi Msaidizi 2: Mwarabu Mumba (Morogoro)
Mwamuzi wa Akiba: Israel Nkongo (Dar es Salaam