Hapa kazi tu
Shirikishola soka barani Ulaya Uefa limepanga kuviadhibu vyama vya soka vya mataifa ya Ujerumani na Ureno kufuatia matukio mawili yaliyotendwa kwenye mchezo wa nchi hizo kuwania kombe la mataifa ya Ulaya huko Poland na Ukrain.
Uefa imesema kuwa chama cha soka cha Ujerumani kinakabiliwa na kesi ya mashabiki wake kutupa makombora uwanjani wakati wenzao wa Ureno wakikabiliwa na adhabu kufuatia timu yao ya taifa kuchelewa kurudi uwanjani kipindi cha pili cha mchezo huo ambao Ujerumani ilishinda goli 1 kwa 0.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa kamati ya nidhamu ya Uefa inataraji kukutana alhamisi ya juma hili kujadili juu ya sakata hilo ambalo limekuja ikiwa ni siku chache tuu baada ya mashindano hayo kuanza.
0 comments:
Post a Comment